STRIKA
USILIKOSE
Tuesday, October 29, 2013
Yanga kuvuna nini kwa Mgambo JKT, kazi ipo jijini Mbeya
WAKATI watani wao wa jadi Simba ikipokea kipigo cha kwanza kwa msimu huu mbele ya Azam, mabingwa watetezi Yanga jioni ya leo inatarajiwa kuvaana na Mgambo JKT katika mfululizo wa Ligi Kuu.
Yanga yenye pointi 19 itahitaji ushindi kwa Mgambo ili kujiweka pazuri katika msimamo wa ligi hiyo baada ya jana wapinzani wao wa jadi kuboronga na kuruhusu kipigo cha kwanza, lakini bado itakuwa ikiiombea Mbeya City isiendeleze wimbi la ushindi itakapoumana na Prisons kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya.
Ushindi wowote wa Mbeya City utamaanishja Yanga itasalia kwenye nafasi ya tatu ikiiengua Simba tu ambayo kwa sasa ipo nafasi ya pili.
Mbeya City ina pointi 20 sawa na Simba ila inazidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufunga na ushindi mbele ya Prisons iutaifanya walingane na Azam na kuendelea kukaa kileleni wakati Yanga ikishinda itafikisha pointi 22.
Hata hivyo Yanga tayari imetangaza wazi kuwa inachohitaji kwa sasa ni ushindi kwa mechi zake zilizosalia bila kujali kama itamaliza duru hilo katika nafasi ipi.
Mabingwa watetezi hao iliyosaliwa na mechi zake zote dhidi ya maafande wa JKT, ilikatishwa wimbi lake la ushindi Okti\oba 20 baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na Simba.
Yanga pengine itataka kupata ushindi mnono kama ilivyofanya mtani wake wealipoitandika maafande hao mabao 6-0 huku Amissi Tambwe akitiupia kambani mabao manne pekee yake.
Ingawa kocha wa Mgambo, Mohammed Kampira alisema leo watashuka dimbani kwa nia ya kuidhibiti Yanga akiwategemea vijana wake wa U20.
Ukiondoa pambano la Dar, macho na masikio ya mashabiki wa soka yanaelekezwa jijini Mbeya kwenye pambano la kukata na nmundu baina ya wenyeji wa mkoa huo Mbeya City na Prisons.
Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu inaonekana ndiyo kipenzi cha mashabiki wengi wa jiji hilo, huku Prisons ambao ni wazoefu wa ligi 'wakisuswa' kwa kile kinachoelezwa kuwa imezidi kulowea Dar, kitu ambacho leo inatarajiwa upinzani mkali baina ya timu hiyo na mgawanyo wa mashabiki.
Hiyo ni moja ya mechi tatu zinazochezwa leo nyingine ikiwa ni zile za maafande wa JKT Ruvu itakayokuwa ugenini dhidi ya Rhino Rangers kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Baada ya matokeo ya mechi za jana zilizoshuhudia Mtibwa Sugar wakikandamizwa mabaop 3-0 na Coastal Uinon, Ruvu Shooting na Kagera Sugar zikitoshana nguvuya kufungana bao 1-1 na Ashanti United kudinda ugenini dhidi ya Oljoro JKT, kuna mabadiliko katika msimamo huo kama inavyoonekana hapo chini.
Pia Kipre Tchetche aliyekuwa mfungaji wa mabao yote ya Azam jana wakati wakiizamisha Simba amekwea hadi nafasi ya tatu ya wafungaji bora akiwa na mabao sita, mawili pungufu na ya kinara aliyedhibitiwa, Amissi Tambwe.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
01. Azam 11 6 5 0 17 7 10 23
02. Simba 11 5 5 1 21 10 11 20
03. Mbeya City 10 5 5 0 13 7 6 20
04. Yanga 10 5 4 1 21 11 10 19
05. Ruvu Shooting 11 4 4 3 13 10 3 16
06. Kagera Sugar 11 4 4 3 11 8 3 16
07. Mtibwa Sugar 11 4 4 3 16 15 1 16
08. Coastal Union 11 3 6 2 10 6 4 15
09. JKT Ruvu 10 4 0 6 9 11 -2 12
10.Ashanti 11 2 4 5 10 19 -9 10
11.Prisons 10 1 5 4 5 12 -7 8
12.Rhino Rangers 10 1 4 5 8 15 -7 7
13.Oljoro 11 1 4 6 8 16 -8 7
14.Mgambo 10 1 2 7 3 18 -15 5
Wafungaji:
8- Tambwe Amisi (Simba)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Hamis Kiiza (Yanga)
6- Kipre Tchetche (Azam)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Themi Felix (Kagera)
4- Didier Kavumbagu (Yanga), Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union)
3- Jerry Tegete, Mrisho Ngassa (Yanga), Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John (Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Khamis Mcha (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Aggrey Morris, John Bocco, Joseph Kimwaga, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Peter Mapunda, (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), John Matei, Mwinyi Ally (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment