Bale na Ronaldo |
Zlatan Ibrahimovic |
MCHEZAJI ghali kwa sasa Gareth Bale, ni miongoni mwa wachezaji 23 akiwamo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi watakaowania Tuzo ya FIFA cha Mchezaji Bora Duniani (FIFA's Ballon d'Or).
Aidha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, Jose Morinho wa Chelsea na Alex Ferguson ni kati ya makocha watakaowania tuzo ya Kocha Bora wa Dunia wa FIFA.
Winga huyo (23) amejumuisha katika orodha ya awali ya watakaowania tuoz hiyo inayotolewa kila mwaka ambayo kwa sasa inashikiliwa na Messi.
Mkali huyo aliteua Real Madrid msimu huu akitokea Tottenham Hotspur, alivunja rekodi ya kuwa mchezaji mwenye uhamisho ghali akipiku rekodi ya Ronaldo kwa kunyakuliwa na Madrid atapigana kumbo na Mchezaji Bora wa Ulaya, Franck Ribery.
Orodha kamili iliyotangazwa na FIFA kuwania tuzo hiyo ni kama ifuatavyo;
Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris Saint-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer, (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).
Orodha kamili ya makocha watakaochuana katika tuzo hizo za FIFA ni pamoja na Carlo
Ancelotti (Paris Saint-Germain), Rafael Benitez (Napoli), Antonio Conte
(Juventus), Vicente del Bosque (Spain), Alex Ferguson (formerly
Manchester United), Jupp Heynckes (formerly Bayern Munich), Jurgen Klopp
(Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari
(Brazil), Arsene Wenger (Arsenal)
No comments:
Post a Comment