STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 30, 2013

Simba, Kagera Sugar kesho hapatoshi Dar

Kagera Sugar
Simba
 LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya 12 kesho kwa pambano kati ya Simba na Kagera Sugar, mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar  es Salaam.
Pambano hilo ni fursa kwa Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi japo kwa muda, kwani iwapo atashinda itafikisha pointi 23 na kulingana nma vinara wa sasa Azam na Mbeya City.
Katika mechi yao iliyopita Simba ilikula kichapo kwa Azam kwa mabao 2-1 na kuwatoa kileleni, hivyo huenda kesho itaikaribisha Kagera kwa hasira ili kuweza kurudi kwenye ufalme wake kabla ya kusubiri kuangalia watani zao Yanga watafanya nini Ijumaa watakapovaana na JKT Ruvu.
Mshambuliaji nyota Amissi Tambwe ambaye hakucheza katika pambano lililopita na kumpa wakati mgumu 'pacha' wake, Betram Mombeki inaelezwa huenda akashuka dimbani kesho na kuendeleza kazi yake ya mabao ili kumkimbia Hamis Kiiza 'Diego' wa Yanga aliyemfikia jana baada ya kufunga bao Yanga ilipoilaza Mgambo JKT mabao 3-0.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment