STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, November 3, 2013

Azam, Mbeya City yaziporomosha Yanga, Mtibwa yazinduka

Azam wakishangilia moja ya mabao yao ya jana

Mbeya City
BAO la kujifunga la beki wa Ashanti United, Samir Luhava, lilitosha kuifanya Mbeya City kuendeleza rekodi ya kushinda mechi mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayoicheza kwa mara ya kwanza na kurejea kwenye nafasi ya pili nyuma ya Azam waliorejea kileleni baada na wao kupata ushindi wa mabao 3-0.
Mbeya City, iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Sokoine inadaiwa haikuonyesha soka lake lilizoeleka kutokana na kubanwa na Watoto wa Jiji, Ashanti ambao walioinyesha walienda Mbeya kufuata ushindi.
Hata hivyo dakika ya 30 ya pambano hilo, Samir katika harakati za kuokoa mpira langoni kwake alijikuta akijifunga bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Ashanti kurejea Dar kinyonge kusubiri kuumana na Simba siku ya JUmatano.
Nao Azam waliendelea kuonyesha dhamira yao ya kuwa mabingwa wapya nchini baada ya kuinyoa Ruvu Shooting mabao 3-0 na kuiporomosha Yanga hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu kwa kurejea kileleni ikifikisha pointi 26.
Mabao ya Azam iliyokuwa uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi yalifungwa na Kipre Tchetche, Joseph Kimwaga na Mcha Khamis 'Vialli'.
Mtibwa Sugar baada ya kukumbana na kipigo cha mbwa mwizi uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mechi iliyopita jana ilizinduka na kuinyoa Rhino Rangers kwa bao la Salim Mbonde huku, Coastal Union na Mgambo JKT zilishindwa kutambiana kwa kutoka suluhu.
Ligi hiyo itaendelea tena kwa pambano moja tu la kukamilisha mechi za raundi ya 12 kwa timu ya Prisons Mbeya kuialika Oljoro JKT kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

No comments:

Post a Comment