Amissi Tambwe (kulia) Kinara wa mabao Ligi Kuu akiwa na bao 9 |
Hamis Kiiza 'Diego' anayefuata kwa magoli mengi |
Mabao 10 kati hayo mabingwa hao walipata katika mechi zao tatu mfululizo zilizochezwa hivi karibuni dhidi ya timu za maafande.
Yanga ikiwa na magoli 28 ya kufunga yenyewe imeruhusu mabao 11 na kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa 17 ikizizidi timu nyingine 13 zinazoshiriki ligi hiyo inayomaliza duru la kwanza wiki ijayo.
Simba walio kwenye nafasi ya nne katika msimamo huo ndiyo inayowafuata Yanga kwa kufumania nyavu mara nyingi ikiwa na mabao22 na kufuatiwa na Azam kisha Mtibwa Sugar zenye mabao 20 na 17.
Mabingwa wa zamani wa soka Tanzania, Coastal Union ndiyo timu yenye safu ngumu katika ligi hiyo ikiwa imeruhusu mabao sita mpaka sasa ikifuatiwa na timu za Azam na Mbeya City zenye kufungwa mabao 7 kila moja.
Timu yenye ukuta mwepesi katika ligi hiyo ni Mgambo JKT iliyofungwa mabao 21 na kufuatiwa na Ashanti United iliyoruhusu mabao 20.
Safu butu ya ushambuliaji katika ligi hiyo ni Mgambo yenye mabao matatu tu ikifuatiwa na Prisons Mbeya ambayo jioni hii inashuka dimbani kuwakaribisha Oljoro JKT katika mechi ya mwisho ya raundi ya 12.
Mpaka sasa ligi ikiwa imebakiza mzungumko mmoja kabla ya kumaliza duru la kwanza jumla ya mabao 182 yamefungwa na timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Azam yenye pointi 26 sawa na Mbeya City zinazotofautishwa na uwiano wa mabao iliyonayo.
Mshambuliaji Amissi Tambwe wa Simba akiendelea kuongoza akiwa na mabao 9 akifuatiwa na Hamis Kiiza 'Diego' wa Yanga mwenye magoli 8.
Yanga iliyokuwa kileleni imerejea nafasi ya tatu ikiwa na pointi 25 kisha Simba wakifuatia na pointi zao 21, wakifuatiwa na Mtibwa Sugar ambayo ushindi wa jana dhidi ya Rhino Rangers umewafanya wafikishe pointi 19.
Kagera Sugar yenye ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 17 na Ruvu Shooting iliyofungwa na Azam jana imeporomoka toka nafasi ya sita hadi ya nane ikiwa na pointi 16 sawa na Coastal ambayo sare yake ya jana dhidi ya Mgambo imechupa hadi nafasi ya saba.
Mgambo imeendelea kuburuza mkia ikiwa na pointi sita ikifuatiwa na Oljoro yenye pointi 7 na Prisons yenye pointi 8, japo yoyote kati ya timu hizo inaweza kuchupa toka nafasi ilizopo kama moja wapo itashinda kwqenye uwanja wa Sokoine-Mbeya watakapoumana jioni hii.
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014
P W D L F A GD PTS
01.Azam 12 7 5 0 20 7 13 26
02.Mbeya City 12 7 5 0 16 7 9 26
03.Yanga 12 7 4 1 28 11 17 25
04.Simba 12 5 6 1 22 11 11 21
05.Mtibwa Sugar 12 5 4 3 17 15 2 19
06.Kagera Sugar 12 4 5 3 12 9 3 17
07.Coastal Union 12 3 7 2 10 6 4 16
08.Ruvu Shooting 12 4 4 4 13 13 0 16
09.JKT Ruvu 12 4 0 8 9 16 -7 12
10.Rhino Rangers 12 2 4 6 9 16 -5 10
11.Ashanti 12 2 4 6 10 20 -10 10
12.Prisons 11 1 5 5 5 14 -9 8
13.Oljoro 11 1 4 6 8 16 -8 7
14.Mgambo 12 1 3 8 3 21 -18 6
Wafungaji:
9- Tambwe Amisi (Simba)
8- Hamis Kiiza (Yanga)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Kipre Tchetche (Azam)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Themi Felix (Kagera), Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa (Yanga)
4-Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union), Jerry Tegete (Yanga)
3- Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union), Mcha Khamis (Azam)
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John, Peter Mapunda,(Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Joseph Kimwaga (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo, Mbuyi Twitte, Oscar Joshua (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah, Abbas Mohammed (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah, Aggrey Morris, John Bocco, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Deo Deus (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Kisiga, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), Samir Luhava (OG), John Matei, Mwinyi Ally (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas, Salum Kanoni (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)
Ratiba ya kufungia duru la kwanza:
Nov 06, 2013
JKT Ruvu vs Coastal Union
Ashanti Utd vs Simba
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar
Kagera Sugar vs Mgambo JKT
Nov 07, 2013
Azam vs Mbeya City
Rhino Rangers vs Prisons
Yanga vs Oljoro JKT
No comments:
Post a Comment