Kocha Kim Poulsen |
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa
dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine
16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza
Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Wachezaji
walioitwa ni makipa wanne; Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga),
Deogratias Munishi (Yanga) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey
Morris (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu
Shooting), Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo
wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa)
na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo
ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna
Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano
(Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo
washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga),
Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji
ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP
Mazembe, DRC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
No comments:
Post a Comment