Gervas Kadaga(25) anayetuhumiwa kumuua mkewe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
MAMA mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge
alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika
shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha
Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa
jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe
aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini
hapo.
Tukio hilo limetokea Novemba
21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao
ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa
Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake
ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye
amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.
Hata hivyo Kamanda Athumani
alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo
ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku
mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya
rufaa ya Mbeya alikolazwa.
Akizungumza katika hospitali
ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la
Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja
akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.
Alisema yeye alipewa taarifa
za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa
marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi
na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.
Mama huyo alisema kuwa vijana
hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda
mrefu;
''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana
kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na
mume,''alisema.
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment