James Kisaka enzi za uhai wake |
Kisaka aliyewahi kung'ara katika nafasi ya ukipa ndani ya Simba na klabu nyingine alikuwa amelazwa hospitali wiki kadhaa sasa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza na kutoona na aliakuwa akiendelea kuimariksa.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia tarataibu za mazishi za kipa huyo nyota wa zamani na kocha aliyejizolea sifa kemkem za ufanisi wa kazi yake.
James
Kisaka alizaliwa mwaka 1955 mjini Dar es Salaam na alipata elimu yake
ya Msingi katika shule ya Oysterbay na baadaye sekondari za Mzizima na
Tambaza, Dar es Salaam pia.
Alianza
kupata umaarufu wa soka tangu anasoma na haikushangaza aliposajiliwa na
Sigara akiwa nba umri mdogo.
Baadaye alichezea Nyota Nyekundu, Simba kabla ya kwenda Small Simba ya Zanzibar na baadaye Volcano ya Kenya alipokwenda pamoja na Zamoyoni Mogella na Lilla Shomari na kisha kutua Ndovu ya Arusha.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Simba kilichokwenda ziara ya mafunzo nchini Brazil mwaka 1981.
Kisaka atakumbukwa kwa upole wake na ufanyaji kazi kwa bidii enzi za uhai wake.
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema. Ameen
.
No comments:
Post a Comment