Awadh Juma (kulia0 mmoja wachezaji sita wapya wa Simba. |
KAMATI
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
imekutana Jumamosi (Desemba 28, 2013) kujadili mambo mbalimbali
yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo usajili wa dirisha dogo ambapo klabu
zenye matatizo zimepewa hadi Januari 10 mwakani kurekebisha.
Taarifa
ya TFF, imesema baadhi ya klabu ikiwemo Simba zimezidisha idadi ya
wachezaji, hivyo zimepewa hadi muda huo kupunguza ambapo zikishindwa
kazi hiyo itafanywa na Kamati yenyewe.
Pia klabu nyingine zimetakiwa ama kuvunja mikataba ya wachezaji au kuendelea kuwa nao, na si kuendelea kuwalipa mishahara wakati imeshawaondoa katika orodha yao.
Kuhusu mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyesajiliwa Yanga, TFF imesema inafahamu kuwa klabu ya Simba bado haijalipwa fedha za kumuuza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na itasaidia kufuatilia FIFA fedha za mauzo ya mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment