STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, January 22, 2014

Moto wateketeza wanne wa familia moja Morogoro

Picha haihusiani na taarifa hii
WATU wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya moto kuteketeza nyumba yao wakiwa wamelala usiku wa manane juzi mkoani Morogoro.

Waliofariki ni baba na watoto wake watatu, huku mama yao akijeruhiwa na kulazwa hospitalini.

Tukio hilo lilitokea saa 7:00 usiku jana katika kijiji cha Iputi, wilayani Ulanga.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, Faustine Shilogile jana alisema tukio hilo lilitokea katika eneo la mashambani kwenye kijiji cha Iputi.

Kamanda Shilogile aliwataja waliofariki kuwa ni baba wa watoto hao, Kassim Maleo (42) na watoto wake Kumbukeni Maleo (5), Mwanaisha Maleo (4) na Halfa Maleo (2), wote wakazi wa mashambani kijiji cha Iputi wilayani Ulanga.

Alisema mama wa watoto hao, Kisia Kihina (35), mkazi wa Iputi alinusurika kifo lakini alipata majeraha na kulazwa katika Kituo cha Afya cha Mwaya akipatiwa matibabu.

Kamanda Shilogile alisema tukio hilo lilitokana na familia hiyo kutozima moto wa kuni baada ya kumaliza kupika chakula cha usiku, ambao baadaye ulishika nyumba hiyo na kuiteketeza wakiwa wamelala.

Diwani wa Kata ya Mwaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Furaha Lingeli, alilsema kuwa, hali ya mama wa watoto hao ni mbaya.

Kadhalika, alisema kuwa miili ya marehemu ilizikwa jana kijijini hapo.

Kamanda Shilogile aliwataka wananchi mkoani Morogoro kuwa waangalifu kuhusu moto hususani wanapomaliza kupika na kwamba matukio kama hayo yamekuwa yakitokea katika maeneo ya mashambani ambayo kwa sasa watu wengi wanajishughulisha na kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo.
NIPASHE

No comments:

Post a Comment