Uganda ilipokwaruzana na Zimbabwe na kwenda suluhu ya kutofungana jana |
Burkina Faso na Morocco walipoonyeshana kazi (picha zote Kickoff.com) |
Michezo hiyo yote ilichezwa kwenye uwanja wa Athlone mjini Cape Town, ambapo Waganda na Zimbabwe ndiyo waliotangulia kushuka dimbani kabla ya Morocco kuvaana na Burkina Faso na kushuhudia Morocco wakishindwa kupata ushindi uliokuwa ukionekana dhahiri kwao baada ya Wabukinabe kurejesha goli jioni.
Morocco alitangulia kupata bao dakika ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo huo lililofungwa na El Bahri akimalizia kazi ya El Ouadi, lakini walishindwa kulilinda baada ya Ouedraogo kuifungia Burkina Faso dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo huo na kuambulia pointi moja.
Kwa matokeo hayo ya jana , Uganda imeendelea kuongoza kundi hilo la B ikiwa na pointi nne baada ya mechi yake ya kwanza kuifumua Burkina Faso kwa mabao 2-1 ikifuatiwa na Morocco na Zimbabawe zenye pointi mbili kila moja na Bunikane ikikamata mkia ikiwa na pointi moja tu.
Michuano hiyo itaendelea tena jioni ya leo kwa mechi za kundi C, Libya kupepetana na Ghana na wawakilishi wa CECAFA, Ethiopia iliyolala mbele ya Libya kwa mabao 2-0 itakwaruzana na Jamhuri ya Kongo.
No comments:
Post a Comment