STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 13, 2014

Arsenal yashindwa kurejea kileleni, Adebayor azidi kumuumbua AVB

Emmanuel Adebayor
Steven Gerrard aklifunga mkwaju wa penati dakika za lala salama na kuisaidia Liverpool kushinda 3-2 mbele ya Fulham
Arsenal wakikoswa bao la wazi jana na  Manchester United uwanja wa Emirates
WAKATI mshambuliaji Emmanuel Adebayor akiendelea kumuumbua aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspur, Andre Villas Boas baada ya usiku wa jana kutupia mabao mawili kimiani na kuisaidia Spurs kupata ushindi mnono wa magoli 4-0 ugenini dhidi ya Newcastle Utd, Arsenal wameshindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Engaland baada ya kubanwa na Manchester Utd nyumbani.
Machester United iliyosafiri hadi London ya Kaskazini kuivaa Arsenal walilazimisha suluhu isiyo ya magoli na kuiacha Arsenal ikisalia kwenye nafasi ya pili nyuma ya Chelsea inayoongoza kwa pointi 57, moja zaidi ya vijana wa Gunners.
Adebayor aliyekuwa akiwekwa benchi na AVB wakati Spurs ikifanya vibaya katika ligi hiyo, alionyesha jinsi alivyo muhimu kwa kikosi hicho alipofunga bao la kwanza dakika ya 19 lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili, Paulinho alifunga bao la pili dakika ya 53 kabla ya Adebayor kurejea tena kambani kwa kufunga bao la tatu dakika ya 82 na  Chadli kumalizia udhia katika mbili kabla ya pambano hilo kumalizika kwa kufunga bao la nne lililoinyong'onyesha Newcastle Utd nyumbani kwao.
Ushindi huo umeifanya Spurs kufikisha pointi 50 na kuipumulia Liverpool yernye pointi 53 ambayo jana iliifunga Fulham nyumbani kwao kwa mabao 3-2, mabao yaliyofungwa na Daniel Sturridge, Coutinho na nahodha Steven Gerrard.
Katika mechi nyingine Stoke City na Swansea City zilitoka sare ya 1-1 huku mechi mbili za Everton dhidi ya Crystal Palace na ile ya Man City dhidi ya Sunderland zikiahirishwa kutokana na hali ya hewa mbaya iliyoadhiri miji iliyokuwa ichezwe mechi hizo.

No comments:

Post a Comment