Yebaaa! Watatukoma mwaka huu, Messi na Neymar wakipongezana jana |
Adriano Correia alianza kuiandikia Barca bao dakika ya pili tu ya mchezo huo akimalizia kazi ya Pedro kabla ya Messi kuanza vitu vyake kwa kufunga bao la pili dakika ya 36 kwa pasi ya FÃ bregas, mabao yalidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa wenyeji kuandika bao la tatu kupitia Alexis Sanchez aliyemalizia pasi ya Messi katika dakika ya 53.
Pedro aliiongezea Barca bao dakika tatu baadaye kwa kasi nzuri ya Fabregas ndipo Messi aliporejea tena kambani kwa kufunga bao lake la pili lililokuwa la tano kwa Barca akisaidiwa na Sánchez na msumari wa mwisho ukapigiliwa na Neymar dakika moja kabla ya kumalizika kwa mchezo huo na kuirejesha Barcelona kileleni ikiitoa Atletico Madrid waliokuwa wamekaa baada ya jana kushinda mabao 3-0 dhidi ya Real Valladorid.
Timu zote zimelingana pointi zikiwa na 60 kila mmoja ila zinatofautisha uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku wakifutiwa kwa karibu na Real Madrid ambayo itashuka dimbani leo ugenini dhidi ya Getafe.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana Levante ilishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Almeria na Celta Vigo imepata ushindi wa mabao 2-0 ugenini leo Jumapili dhidi ya wenyeji wao Villarreal.
No comments:
Post a Comment