WIKI ya tatu mfululizo vurugu zimeendeleakatika kanisa la Moravian baada ya jana tena kuibuka kitimtim katika kanisa la Mwananyamala Msisiri A Kinondoni Dar Es
Salaam.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alilidokeza MICHARAZO kuwa chanzo ilikuwa ni Maaskofu
kutoka makao makuu ya kikanda ambao walifika na kutaka kuingia ndani ya Kanisa
hilo na kuzuiwa na mmoja wa waumini.
Muumini huyo alidai kwamba Maaskofu hao wasiingie
kwani mgogoro uliopo ndani ya kanisa hilo kwani utamalizwa na waumini wenyewe na
kwamba kuwepo kwao kungechochea vurugu zaidi.
Wakati Maaskofu wakipinga amri
hiyo, waumini ambao walikua ndani ikiwa ndio wanaanza ibada ya kwanza walisikia
na ndipo wachache wakatoka nje, wengine wakishinikiza Maaskofu hao waingie huku
wengine wakitaka waondoke.
Mabishano makali yaliyofuatiwa na ngumi yalizukabaina ya pande hizo mbili
hadi maaskari ambao inaonekana walitonywa mapema hivyo kuwa karibu na eneo
la tukio walipoingialia kati na kutuliza mtafaruku huo.
Hata hivyo bado waumini
walishinikiza kutoendelea na ibada hadi Maaskofu wa Kikanda waondoke eneo hilo
na waumini kuamua kubaki nje badala ya kuendelea na ibada, wengine wakitimka kwa kuhofia vurugu zaidi.
Baadhi ya waumini waliokuwa wakiondoka walissikika wakisema kuwa heri wahamie makanisa
mengine kwani hamkani si shwari tena kanisani hapo.
Inasemekana
Maaskofu hao wa Kikanda walifika kanisani hapo ili kuamuru Baraza la Kanisa
hilo kuvunjwa ili kupisha uchaguzi mwingine wa viongozi baada ya Baraza hilo
kutuhumiwa kufuja pesa za kanisa kwa kutowasilisha mahesabu kwa waumini.
Udondozi
zaidi umebaini kwamba kanisa hilo limekuwa na vurugu za chini chini ambazo
inasemekana zimeanzia makao makuu ya Kanisa hilo, huku ikielezwa kwamba kumeibuka
kambi mbili za uhasama, moja ikishinikiza viongozi waliopo sasa waondoke
madarakani huku nyengine ikiunga mkono viongozi hao wabaki hadi uchaguzi mkuu
utakapofanyika.
Chimbachimba zaidi toka kwa shuhuda huyo zimebaini kwamba tatizo la msingi ni uongozi
uliopo madarakani kutowasilisha mahesabu yaliyokaguliwa (Audited Account) ya Kanisa hilo lenye vitega uchumi vingi ikiwemo
Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji.
Mgogoro ambao ulifikishwa hadi Kituo cha
Polisi Oysterbay ambapo viongozi waliamuriwa kufanya mahesabu hayo na leo kuyawasilisha
kwa waumini wao jambo ambalo halikufanyika hadi vurugu zilipoibuka tena.
No comments:
Post a Comment