DROO ya mechi za Robo fainali ya michuano ya Kombe la FA Englabnd imetoka na kuonyesha timu gani itakutana na nani katika hatua hiyo baada ya kufuzu mwishoni mwa wiki.
Arsenal walioing'oa Liverpool wenyewe wataanzia nyumbani dhidi ya Everton iliyoitambia Swansea City kwa kuilaza mabao 3-1.
Hata hivyo kocha wa timu hiyo ya Everton, Roberto Martinez amesisitiza kuwa hawana cha kuogopa watakaposafiri kwenda Emirates kuivaa Arsenal .
Martinez alisema: "Wakati wa upangaji wa ratiba mara zote unatumai kuangukia nyumbani, lakini hilo halijalishi – kama unahitaji kutwaa kombe siku zote lazima ujiandae kukutana na yeyote. Tutahitaji kuwa katika kiwango chetu bora lakini ni kitu ambacho tunahitaji kukitazama."
Kutinga katika hatua hiyo ni hatua nzuri kwa kocha Arsene Wenger ambaye kwa muda mrefu hajashuhudia klabu yake ikinyakua taji lolote ambapo kesho itakuwa vitani barani Ulaya kuumana na watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kuona kama inaweza kunyakua matji matatu kwa mpigo.
Arsenal ipo katika nafasi nzuri ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England ikiongoza kwa sasa mbele ya Chelsea, Manchester City na Liverpool.
Mbali na mechi ya Toffee's na Gunners, pia robo fainali ya FA inaonyesha Brighton & Hove Albion itaumana ama Hull City v Sunderland, Sheffield United v Sheffield Wednesday au Charlton Athletic na Manchester City dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Wigan Athletic.
No comments:
Post a Comment