Twiga Stars, Zambia sasa kukipiga mapema
MECHI
ya pili ya Raundi ya Kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC)
kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) sasa itachezwa
Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es
Salaam.
Twiga
Stars tayari ipo kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia
saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage
inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za
bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.
Shepolopolo
iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa
Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa
mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza
ugenini.
Wachezaji
wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha
Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo,
Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma Mwisendi, Fatuma
Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma
Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia
Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
No comments:
Post a Comment