BENITEZ AIPA CHELSEA TAJI LA EUROPA WAKITUNGUA BENFICA
Chelsea wakishangilia na taji lao usiku wa jana |
Kocha Rafa Benitez akiwa ameshikilia taji hilo la Europa League |
Branslav Ivanovic akiifungia Chelsea bao la pili |
Bao la dakika za ziada la pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Amsterdam Arena, lilitumbukizwa kimiani kwa kichwa na beki kutoka Serbia Branslav Ivanovic akiunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Juan Mata.
Kabla ya bao hilo timu hizo zilijikuta zikimaliza dakika 45 za awali zikiwa nguvu sawa kwa kutofungana licha ya kwamba Benfica walionyesha soka la kuvutia wakiwakimbiza Chelsea kabla ya kujikuta kipindi cha pili wakianza kwa kutunguliwa bao kupitia Fernando Torres kuipangua ngome ya Benfica akiwamo kipa wao na kuutumbukiza wavuni katika dakika ya 60.
Hata hivyo dakika nane baadaye Benfica walirejesha bao hilo kwa mkwaju wa penati iliyopigwa kiufundi na nyota wa timu hiyo Oscar Cardozo na kuonyesha huenda mwechi hiyo ingeisha kwa sare ndani ya dakika 90 kabla ya Ivanovic kubadilisha matokeo dakika moja kabla ya dakika tatu za ziada kumalizika.
Hilo ni taji la pili kubwa kwa Chelsea kwa miaka miwili mfululizo, baada ya mwaka jana kutwaa taji la Ligi ya Ulaya ikiwa na kocha Roberto Di Matteo ambapo hata hivyo mwaka huu walishindwa kulitetea na kujikuta wakitupwa kwenye Europa na kufanya kweli kwa kulitwaa licha ya kocha Benitez kuwa na bahati mbaya ya kutokubalika tangu aliporithi nafasi ya Di Matteo.
No comments:
Post a Comment