John Terry akipambana dhidi ya mchezaji wa Villa |
Willian akiwa chini na mchezaji wa Aston Villa |
Chelsea waliokuwa wakihitaji ushindi ili kuzidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo na kuzikimbia timu zinazoifukuzia, walishindwa kuonyesha makeke yao kwa Villa kwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nguvu sawa ya bila kufungana.
Kipindi cha pili kiliendelea kuwepo kwa kosa kosa za hapa na Willian kulitolewa nje baada ya kuonyesha kadi ya pili ya njano na kufuatiwa na nyekundu dakika ya 68 kabla ya wenyeji kujiandikia bao lao hilo la pekee lililofungwa na Fabian Delph katika dakika ya 82 na kuwakata maini vijana wa Jose Mourinho waliokuwa wakisaka ushindi wa nne mfululizo katika EPL.
Dakika za nyongeza za mchezo huo Ramires alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu na wakati kocha wake akienda kuzungumza uwanjani akajikuta naye akitolewa nje kwa kadi kama hiyo nyekundu.
Kwa kipigo hicho Chelsea imesaliwa na pointi zake 66 na kutoa nafasi nzuri kwa wapinzani wake Liverpool na Arsenal ambazo kesho zitakuwa viwanja tofauti kupunguza pengo la pointi. Timu hizo zina pointi 59 kila moja moja pungufu na ilizonazo Manchester City waliopo nafasi ya pili kwa sasa.
No comments:
Post a Comment