IKIWA
imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,
Iringa Vijijini, Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya
leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota, Iringa Vijijini kwa
tuhuma za kugawa Fedha kwa wanakijiji hao, akijua fika Wananchi hao
wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho
siku ya jumapili.
Pichani
shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Rose Kamili akielekezwa sehemu
ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa
jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa
Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa
kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya
jumapili.
Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge
wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara
baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya
Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji
Gari
ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa
kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi
wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria. PICHA NA MICHUZI JR
No comments:
Post a Comment