STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 10, 2014

Japanese anogewa ughaibuni

Japanese kikazi zaidi

Amina Ngaluma 'Japanese' akifurahia maisha Ughaibuni
MUIMBAJI nyota wa zamani wa bendi mbalimbali nchini ikiwamo Double M Sound, African Revolution 'Wana Tamtam', Amina Ngaluma 'Japanese' amesema hana mpango wa kurejea nchini kwa sasa kutokea ughaibuni anakofanya shughuli zake za muziki na bendi ya Jambo Survivors kwa madai muziki wa Tanzania umejaa 'wizi mtupu'.
Akizungumza na MICHARAZO kutoka Thailand walipoweka maskani yao ya kudumu, Ngaluma alisema haoni ya sababu ya kurudi nyumbani kwa sasa wakati maisha yamemnyookea ughaibuni akiwa na bendi hiyo inayopiga muziki asilia na iliyoweka maskani ya kudumu nchini humo.
"Kwa kweli sifikirii kurudi nyumbani leo wala kesho, hii ni kutokana na kuona tofauti kubwa ya kuthaminika kwa wanamuziki kati ya huko na hapa tulipo tukiendeleza makamuzi na bendi ya Jambo Survivors," alisema Japanese aliyetamba na wimbo wa 'Mgumba II'.
Ngaluma alisema muziki wa Tanzania umeshindwa kuwanufaisha wanamuziki wake kutokana na kuwapo kwa unyonyaji kuanzia kwa wamiliki wa bendi mpaka wadau wanaousimamia kama wasambazaji na hata wananchi wanaowaibia wasanii kazi zao bila kujali wala kuwahurumia wanavyovuja jasho lao.

No comments:

Post a Comment