Samuel Sitta akiwa na fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti Bunge Maalum la Katiba |
WAKATI
uchaguzi wa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalumu la Katiba ukitarajiwa
kufanyika leo, wagombea wawili waliojitokeza kutaka kuwania nafasi hiyo,
wameenguliwa baada ya ya kushindwa kurudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa
muda uliopangwa
Wajumbe
hoa Dk Theria Uvisa pamoja na Danstan Chipaka walienguliwa katika kinyang’anyiro
hicho kufuatia kushindwa kurudisha fomu za kugombea ambazo zilipaswa kurudishwa
leo saa 4 asubuhi.
Kufuatia
kuenguliwa kwa wajumbe hao, nafasi hiyo itawaniwa na Samwel Sitta pamoja na Hashim Rungwe ambao ndiyo waliokidhi
vigezo kwa kuchukua fomu na kurudisha kwa wakati.
Uchaguzi
wa Mwenyekiti unatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni, ambapo baada ya
kutangazwa matokeo kutatangazwa uchukuaji fomu kwa wajumbe watakaotaka kuwania
nafgasi ya umakamo mwenyekiti.
Mpaka sasa
anayetajwa kutarajiwa kuwania nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, ni Samia
Suruhu.
Kwa mujibu
wa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Makamu Mwenyekiti wa Bunge anapaswa kutoka
upande wapili wa muungano iwapo Mwenyekiti atakuwa amechaguliwa kutoka upande
mwingine wa muungano hili kuleta usawa.
FK
No comments:
Post a Comment