STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 9, 2014

Taifa Stars sasa kutumia jezi za Adidas


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kwamba kufuatia makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars), zikiwemo jezi ambazo zilianza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Amesema vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
“TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,”amesema Malinzi.
Mwezi uliopita, Malinzi alikwenda makao makuu ya CAF, Cairo nchini Misri kujitambulisha baada ya kurithi kiti cha Leodegar Tenga Desemba mwaka jana na akiwa huko alikutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou aliyeahidi kumpa sapoti kubwa.

No comments:

Post a Comment