LICHA ya awali kuelezwa hafurahii maisha ndani ya Manchester City hasa baada ya kukerwa na viongozi wake kuipuuza sikua yake ya kuzaliwa, Kiungo nyota wa mabingwa hao wa soka wa England, Yaya Toure amesema hana mpango wa kuondoka katika timu hiyo.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba mahasimu wa City, Mashetani Wekundu Manchester United walikuwa wakimvizia ili kumnyakua, lakini mchezaji huyo ameweka bayana kwamba atasalia klabuni hapo kwa msimu
mwingine ujao.
Toure alinukuliwa na kituo cha Sky Sport kuwa mashabiki
wa timu hiyo wamekuwa wema kwake na kwa familia hivyo ameona ni bora
abaki kwa ajili yao.
Vyombo vya habari vimekuwa vikimhusisha kiungo huyo
kuhamia katika vilabu mbalimbali toka wakala wake Dimitry Seluk
alipoandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa
nyota huyo hajatulia.
Seluk alitoa madai kuwa nyota huyo wa kimataifa wa
Ivory Coast hakupewa utambulisho rasmi na klabu katika siku yake ya
kuzaliwa wakati wa safari yao ya Abu Dhabi huku Toure mwenyewe akiunga
mkono kauli hiyo.
Toure amesema kwa sasa mambo yote yako sawa na baada ya
tetesi nyingi kuzungumziwa juu yake anajipanga kufanya kitu kwa ajili ya
mashabiki.
Nyota huyo alijiunga na City akitokea Barcelona mwaka 2010 na
haraka alijitengenezea jina na kuwa mchezaji tegemeo akiisaidia City Kombe la FA mwaka 2011 na mataji mawili ya Ligi
Kuu mwaka 2012 na 2014.
No comments:
Post a Comment