Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa
Interpol nchini Uganda Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo
litarudishwa Nairobi.Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano
usiku mjini Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano wiki jana.
Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah
Esipisu alikanusha habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na
ulinzi wa Rais Kenyatta bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi.
Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa
wa polisi aliyeripoti kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa
Rais.Afisa huyo wa polisi pia alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa
polisi wa ulinzi wa Rais.
Tukio la wizi wa gari hilo,
lilisababisha taharuki miongoni mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari
ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa kuwa na ulinzi mkali.
Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo mtu yeyote anaweza kuathirika.
BBC
BBC
No comments:
Post a Comment