STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 2, 2014

Miyeyusho kuyeyushana na Emilio Mkwakwani Nov 5

Miyeyusho na Emilio katika pozi
Wakitunishiana misuli
BONDIA machachari wa ngumi za kulipwa anayeshikilia mataji ya WBF na UBO, Francis Miyeyusho anatarajiwa kupanda ulingoni jijini Tanga kuzipiga na Mtanzania anayepigana nchini Kenyam Emilio Norfat.
Mabondia hao watapambana katika pigano la uzito wa Feather (kilo 57) siku ya Novemba 5 kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mratibu wa pambano hilo Anthony Rutta alisema maandalizi yameanza kwa kumalizana na mabondia hao wenye sifa zinazolingana kwa sasa katika medani ya ngumi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
"Mabondia Francis Miyeyusho na Emilio Norfat wanatarajiwa kupanda ulingoni kupigana kwa mara ya kwanza Novemba 5 na watasindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi siku hiyo," alisema Rutta.
Rutta alisema itakuwa mara ya kwanza kwa Miyeyusho kupanda ulingoni mkoani Tanga sawa na ilivyo kwa Emilio anayeshikilia nafasi ya pili nchini katika uzito huo wa Feather kati ya mabodia 60.
Emilio anashikilia kwa sasa taji la Afrika Mashariki na Kati la WPBC na rekodi zinaonyesha amecheza michezo 27 akishinda 23 na kupoteza minne, wakati Miyeyusho amecheza 51 ameshinda 38 na kupoteza 11 na kudroo miwili..
Pambano la mabondia hao litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST) ambalo Rutta ndiye Katibu Mkuu wake.

No comments:

Post a Comment