Wachezaji wa Arsenal wakishangilia bao lao kwa kumfuta kiatu Aaron Ramsey |
Podolski akifunga bao la kwanza la Arsenal |
Wachezaji wa Juventus walifurahia baada ya timu yao kufuzu hatua ya 16 Bora |
Hureeee! |
Monaco nao walikuwa na furaha yao kama hivi |
Bayer Leverkusen naop wamefuzu 16 Bora |
Podolski aliiandikia The Gunners bao la kuongoza dakika ya tatu tu tangu kuanza kwa pambano hilo kabla ya Ramsey kuongeza la pili dakika ya 11 na kisha kurudi tena kambani dakika ya 29.
Kipindi cha pili wenyeji walicharuka na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi lililofungwa na mkongwe Wesley Sneijder kwa mpira wa adhabu ndogo katika dakika ya 87.
Dakika tatu baadaye Ramsey alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne na la pili kwake katika mchezo huo na kuifanya Arsenal ikitinga hatua ya 16 Bora nyuma ya Borussia Dortmund ya Ujerumani ambayo ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Anderlecht ya Ubelgiji.
Vijana hao wa Arsene Wenger wana hatari ya kukutana na moja ya timu mojawapo kati ya Real Madrid, Atletico Madrid, Barcelona, PSG, Bayern Munich, Porto au Monaco katika hatua ya mtoano.
Bao la Dortmund lilifungwa na Ciro Immobile katika dakika ya 58 kabla ya wageni kuchomoa dakika sita kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kupitia kwa Aleksandar Mitrovic kwa njia ya kichwa.
Dortmund imeongoza kundi hilo kwa sare hiyo kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, lixcha ya kulinga pointi 13 na Arsenal.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Juventus ikiwa nyumbani ililazmisha suluhu kwa Atletico Madrid na zote mbili kufuzu kwa hatua ya 16 Bora kutoka kundi A, licha ya Olympiakos Pirates kupata ushindi mnono wa mabao 4-2 djhidi ya Malmo ya Sweden.
Nayo timu ya Monaco ya Ufaransa ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kuilaza Zenit St Petersburg ya Russia kwa mabao 2-0 na kuongoza kundi C ambalo lilishuhudia Bayer Leverkusen wakifuzu nao licha ya kung'ang'aniwa ugenini na Benfica ya Ureno.
ZILIFUZU 16 BORA
Kundi A: Atletico Madrid na Juventus
Kundi B: Real Madrid na Basle
Kundi C:Monaco na Bayer Leverkusen
Kundi D: Borussia Dortmund na Arsenal
No comments:
Post a Comment