Nahodha Steven Gerrard haamini kilichoikuta timu yake jana usiku |
Basle wakishangilia bao lao lililofungwa na Frei |
Nenda nje sitaki uhuni uwanjani |
Ronaldo akipongezwa na wenzake |
Medran akifunga bao la nne la Real Madrid |
Ushindi huo umeiwezesha Real madrid kuongoza kundi hilo, wakati Liverpool iliyokuwa ikihitaji ushindi ili kusonga mbele imeishia kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Basle ambayo sasa inaungana na Real madrid kusonga mbele baada ya sare ya ugenini.
Liverpool wakiwa kwenye uwanja wao wa Anfield walishshtukizwa na wageni wao kwa kufungwa bao katika dakika ya 25 kupitia Fabian Frei na kulazimika kulichomoa katika kipindi cha pili baada ya Lazar Markovic kufunga katika dakika ya 60 na kuongoza msimamo wa kundi B.
Katika pambao jingine la kundi hilo la B, Real Madrid wakiwa nyumbani waliishindilia Lodogorets kwa mabao 4-0, huku Cristiano Ronaldo akifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Marelonho wa Logorotes kucheza rafu iliyomfanya atolewe nje kwa kadi nyekundu na kumfanya nyota huyo kumfikia gwiji wa zamani wa klabu hiyo Raul Gonzalez kwa idadi ya mabao aliyofunga kwenye michuano hiyo.
Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya 20 na kumfanya kufikisha jumla ya mabao 72 na kusaliwa mabao mawili kumfikia hasimu wake, Lionel Messi mwenye mabao 74, ambaye usiku wa leo atakuwa dimbani tena kuiwakilisha Barcelona dhidi ya timu ya PSG.
Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa naGareth Bale katika dakika ya 38 kabla ya weatokea benchi Alvaro Arbeloa na Alvaro Medran kufunga mabao mengine katika dakika za 80 na 88.
No comments:
Post a Comment