Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama, Juma Protas |
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema
wilaya ya Kahama, Juma Protas alisema tukio hilo lilitokea juzi
katikati ya Kijiji cha Kalagwe kata ya Ntobo na Kijiji cha
Nyambula Kata ya Ngongwa majira ya Saa 3:30 Usiku wakati wakitoka
kwenye Kampeni Kijiji cha Kakola.
Akizungumzia
tukio hilo Protas alisema walipofika eneo la Daraja walikuta
magari matatu yamesimama pembeni ambayo ni Basi la Jordan ambalo
lilikuwa linatoka mkoani Geita kuelekea Kahama,Roli aina ya Fuso na Gari
ndogo inayomilikiwa na Kampuni ya TBL kupitia bia ya Balimi ambayo nayo
yalikuwa yametekwa.
Alisema
wakati wanajaribu kuyapita magari hayo ghafla waliona Mawe na Miti
ambayo ilikuwa imetandazwa barabarani na ndipo majambazi hao waliamuru
Msafara huo ambao ulikuwa na magari mawili wenye watu 10 wasimame na
watoe simu na fedha walizokuwa nazo.
“Tulisikia
sauti wakisema zimeni taa za gari na muziki na hatuwezi kuwadhuru
nyinyi Makamanda ila tunataka fedha na simu, na tupo kazini mnatakiwa
kuwalaumu viongozi waliokula Pesa za Escrow bila hiyo tusingefanya haya
mnayoyaona”alifafanua Protas.
Aliwataja
waliokuwemo kwenye msafara huo kuwa ni mratibu wa Kanda ya ziwa
mashariki Renatus Mzemo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Kanda ya
ziwa Magharibi, Emmanuel Mbise na Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi wa
chama hicho Kanda hiyo Juma Protas ambaye ndiye Mwenyeki wa Chadema.
Viongozi
hao wa Chadema walikuwa wamepanda gari aina ya Toyota Prado yenye no.
T 707 BBP ambayo hata hivyo ilivunjwa baadhi ya vioo.
“Tuliibiwa
fedha tathimini zaidi ya shilingi laki tisa pamoja na simu 11 ambazo
hazikufahamika mara moja thamani yake na gari yetu moja ambayo ni ya
mdau alyejitolea kutusaidia ilivunjwa vioo na ile ya M4C yenyewe
walisema hawawezi kuivunja maana ni wananchi walichanga
kuinunua”,aliongeza Protas
“Kulikuwa
na magari mengi tuliyoyakuta yametekwa na abiria walinyang’anywa simu
na fedha zao, pia kulikuwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Lunguya
ambaye alitekwa akiwa na pikipiki na wakamfunga Kwenye mti pamoja na
ddugu yake na baada ya kuchukua fedha walitoweka
kusikujulikana”,AliongozeaMwenyekiti huyo.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama lilifika eneo hilo baada ya
kupewa taarifa na abiria waliokuwa kwenye basi ambalo lilitekwa na
kukuta majambazi hayo yakiwa yametokomea kusikojulikana na kutoa msaada
wa kiusalama kwa magari yote na abiria waliotekwa.
MALUNDE
No comments:
Post a Comment