RAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Fainali za Mashindano ya Kombe la Kawambwa 2014 itakayochezwa Desemba 20 mjini Bagamoyo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa michuano hiyo, Masau Bwire michezo ya nusu fainali za michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kuanzia Ijumaa kwa kuzikutanisha timu za Zing Zong na Mwambao.
Pambano la pili la nusu fainali za michuano hiyo itazikutanisha timu za Mapinga heroes dhidi ya New Stars na mechi zote zitakchezwa kwenye uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Bwire alisema washindi wa mechi hizo za nusua fainali watakutana kwenye fainali itakayochezwa Desemba 20 na mgeni rasmi atakuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Alisema kuwa mbali na Malinzi pia fainali hizo zinatarajiwa kuhudhuria na viongozi wengine mbalimbali walioalikwa na kutakuwa na michezo mimngine ya kusisimua katika kupamba fainali hizo.
Miongoni mwa michezo itakayochezwa siku hiyo ni pamoja na ile ya kuvuta kamba kwa wazee, kukimbiza kuku na kina mama kukimbia kwenye magunia mbali na burudani ya ngoma na Bongofleva.
Mshindi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa atanyakua Kombe kubwa na zawadi wa Pikipiki huku timu nyingine zikipata vikombe na zawadi nyingine ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment