STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 26, 2013

Singano kutovimba kichwa kwa sifa apewazo

Ramadhani Singado 'Messi'
WINGA machachari wa Simba, Ramadhani Singano 'Messi' amesema pamoja na sifa na pongezi anazomwagiwa na mashabiki wa soka kutokana na kuongeza kiwango katika siku za karibuni, hatabweteka na kuvimba kichwa badala yake atazidi kujituma ili aweze kutimiza ndoto za kutamba kimataifa.
Aidha, mchezaji huyo aliyeng'ara kwenye pambano la Nani Mtani Jembe, na kusaidia Simba kuicharaza Yanga mabao 3-1, amewataka wachezaji wenzake kuzingatia mazoezi, kujituma, kujitunza na kuzingatia nidhamu ndani na nje ya uwanjani iwapo wanataka kufika mbali.
Akizungumza na MICHARAZO katika mahojiano maalum juzi, Messi alisema anawashukuru wote wanaompongeza na kummwagia sifa kwa kung'ara pambano la Simba na Yanga, lakini alisema anachukua pongezi hizo kama changamoto kwake za kuongeza juhudi ili afike mbali zaidi.
Singano alisema hawezi kubweteka na kuvimba kichwa kwa pongezi hizo kwa kutambua kuwa mashabiki wa soka ni 'vigeugeu' wanaoweza kumgeuka wakati wowote atakapocheza chini ya kiwango, pia malengo yake ni kufika mbali zaidi na mahali alipo sasa.
"Nawashukuru wanaonimwagia pongezi, namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa hivi nilivyo pamoja na makocha na wachezaji wenzangu, ila siwezi kubweteka badala yake nitajituma zaidi ili nifike mbali," alisema.
Singano alisema kiu yake siyo kucheza Simba tu na Taifa Stars, bali kucheza soka la kulipwa kitu anachoamini anaweza kutimiza kwani uwezo anao na hasa akimtegemea Mungu kumpa umri na siha njema.
Winga huyo, mmoja wa wachezaji wakiopandishwa kikosi cha kwanza cha Simba kutoka timu B, amekuwa gumzo ndani ya kikosi hicho na Taifa Stars kutokana na uwezo wake wa kupiga chenga, mbio na kufunga.

No comments:

Post a Comment