NDONDI ni miongoni
mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Wapo wanamichezo
waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa
ndondi.
Miongoni mwa
wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield,
Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.
Kwa
hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo
Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli 'Masta' Michael Yombayomba, Stanley
Mabesi 'Ninja' Rashid Matumla, Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na
wengineo wengi.
Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa
zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na
mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania,
Cristiano Ronaldo.
Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James,
wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi
akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe
Bryant.
Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi
kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya
mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu
kwa sasa.
Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa
wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa
siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.
Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo,
zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia
mafanikioi ya akina Mayweather.
Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa
kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa
Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.
Bondia huyo wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha
kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu
yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali
yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia
nyota.
Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super
D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa
wanamasumbwi wa Tanzania.
Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa
nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza
ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.
Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi
ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa
yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.
“Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa
kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie
atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya, Hispania,” anasema Super D.
Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota
wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao
Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na
Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.
Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini
akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia,
lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.
“Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua
mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini
ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,”
anasema.
Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion,
umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango
vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.
Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu
mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa
mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa
hapa nchini kama Mbwana Matumla, Francis
Miyeyusho, Ibrahimu Class' King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo.
Miyeyusho, Ibrahimu Class' King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo.
No comments:
Post a Comment