Steven Kanumba enzi za uhai wake |
Mwanamuziki Christian Bella na Mama yake Kanumba, Flora Mtogoha wakikinadi kitabu cha maisha ya marehemu Steven Kanumba kitakachozinduliwa leo pale Ubungo |
Mtunzi wa kitabu hicho akikitambuliosha kwa wanahabari huku mratibu wa onyesho la uzinduzi, Frank akifuatilia kwa makini |
Taasisi hiyo ya inahusika na masuala ya kusaidia wajane na yatima ilianzishwa ikiwa ni njia ya kumuenzi marehemu Kanumba aliyefariki takriban miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza na wanahabari, mtunzi huyo raia wa Canada mwenye asili ya DR Congo, alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuongea na Mama Kanumba kuhusu ndoto za marehemu Kanumba aliyekuwa akipenda kuwasaidia yatima na alipanga kuwa na taasisi ya kusaidia wajane, lakini alifariki kabla ya kukamilisha ndoto zake.
“Mimi nilikuwa mpenzi wa kazi za Steven Kanumba baada ya kufariki niliumia sana, lakini nikafikiria ni jambo gani ambalo naweza kulifanya ili Kanumba aendelee kuishi japo hatupo naye kimwili lakini kiroho tupo naye,” alisema
“Nilifikiria kuandika kitabu kama sehemu ya heshima yangu kwake shujaa huyu kwetu sisi watu tunaopenda kazi zake, kwani Kanumba kanisaidia kujua kuongea Kiswahili kupitia filamu zake, hivyo napenda kuwe na kitu cha kumkumbuka," alisema Zirimwabagabo aliyetoa kitabu hicho kwa lugha mbili, cha Kiswahili na Kiingereza.
Naye Mama Kanumba, alitoa shukrani zake na akisema hakuwahi kufikiria kama mwanaye alikuwa na thamani kubwa kama hiyo hadi watu wa mataifa mengine kuja kuona kama ni mtu ambaye anatakiwa kuwekewa kumbukumbu kwa kuwekewa kitu au taasisi.
Kitabu hicho cha maisha ya kanumba kitazinduliwa kesho kwenye ukumbi wa Landmark Hotel, Ubungo ambako sherehe hizo zitaenda sambamba na uzinduzi wa taasisi hiyo ya Kanumba Foundation chini ya uratibu wa muigizaji Mohammed Mwikongi 'Frank' na burudani itakayosindikiza uzinduzi huo itatolewa na muimbaji Christian Bella.
No comments:
Post a Comment