Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova |
JESHI la Polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road
wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki
katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni
tofauti kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP
ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo
haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na
vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo
polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada
ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa
mbaya zadi.
Kufuatia tukio hilo waandishi wa habari wamezunguka maeneo mbalimbali ya jiji
yaliyodaiwa kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo
ya magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi
kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi
na taarifa kusambaa maeneo mengine.
Katika maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia
sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na
ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha
maisha huku wengine wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani
wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili
kuepuka vitendo hivyo.
Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni
kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi
tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za
wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi
la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga
kufanya fujo ili kulipiza kisasi.
via..ITV
No comments:
Post a Comment