NYOTA wa filamu wa Hollywood, Harrison
Ford, anapatiwa matibabu katika Hospitali moja mjini Los Angels baada ya
ndege yake kuukuu kuanguka katika uwanja wa Gofu.
Mcheza filamu huyo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa akiendesha ndege hiyo mwenyewe.Ndege hiyo ndogo ilinasa kwenye mti wakati ilipokuwa ikitua kwa dharura.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema Harrison Ford alikuwa amejeruhiwa, akionekana kuwa na damu iliyotapakaa usoni.
Matabibu wamesema Ford anaendelea vizuri na kuwa hali yake itatengemaa kabisa.
Muigizaji huyo aliyeanza kuigiza tangu mwaka 1966, amewahi kujeruhiwa wakati wa kuigiza filamu zake ikiwamo mgongo mwaka 1983 na baadaye kifundo cha mguu Juni mwaka jana akiitengeneza picha iitwayo 'Star Wars: The Force Awakens'.
Ntyota huyo anasifika kwa uigizaji wake makini wa filamu zilizompa ujiko miongoni wa filamu hizo ni American Graffiti, Star Wars, Apocalypse Now, The Frisco Kid, The Empire Strikes Back, Raiders of the Lost Ark, Blade Runner, Return of the Jedi, Indiana Jones and the Temple of Doom na Witness.
Nyingine ni; The Mosquito Coast, Working Girl, Indiana Jones and the Last Crusade, Regarding Henry, Patriot Games, The Fugitive, Clear and Present Danger, Sabrina, Air Force One, Six Days Seven Nights, What Lies Beneath, K-19: The Widowmaker, Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull, Extraordinary Measures, Cowboys & Aliens, 42, Ender's Game na Paranoia.
No comments:
Post a Comment