Kikosi cha Kano-Pillars ya Nigeria. |
ABUJA, Nigeria
WACHEZAJI watano
wa timu ya Kano Pillars wamejeruhiwa kwa risasi na watu wenye silaha katika
shambulio lililofanywa na kundi la watu wakati wakisarifi kwenda Owerri kwa
ajili ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Nigeria.
"Wachezaji
watano waliojeruhiwa kutokana risasi hizo ni pamoja na Gambo, Ogbonaya, Eneji
Otekpa, Murtala Adamu, na Moses Ekpai," klabu hiyo iliandika katika
mtandao wa Twitter.
"Watu hao
wenye silaha pia walichukua simu za mkononi na vitu vingine vya thamani kutoka
kwa wachezaji ".
Kutokana na tukio
hilo la uvamizi, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Heartland ameahirishwa kwa muda
usiojulikana.
Timu ya Kano ilikuwa
ikisafiri kwa basi ikiwa na watu 25, wakiwemo wachezaji 18, wakati tukio hilo
likitokea saa 7:15 mchana kwa saa za hapa.
Wachezaji watano
waliojeruhiwa walipata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Centre huko Lokoja.
Kano walikuwa
wakijianda kutetea taji la Nigeria, ambapo walianza msimu kwa ushindi dhidi ya Al
Malakia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika raundi ya awali wikiendi iliyopita.
Hatahivyo, bado
haijajulikana kama ratiba ya mabingwa Kano dhidi ya Moghreb Athletic Tetouane Machi
13 itaendelea kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment