BAADA ya kuelekea kumpoteza mshambuliaji wake matata, Robin van Persie, klabu ya Manchester United imepanga kutoa kitika cha pauni Milioni 60 ili kumnasa mshambuliaji wa Kijerumani Thomas Muller.
Muller mwenye umri wa miaka 25 anaichezea klabu ya Bayern Munich na United itamsajili Mjerumani huyo kama mbadala wa RVP ambaye anatarajiwa kuuzwa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki. Klabu hiyo ya Uturuki imekubaliana na Mashetani Wekundu kulipa dau la Pauni Milioni 4.7 kama ada ya uhamisho wa RVP ambaye atafanyiwa vipimo vya afya wikiendi hii na kusaini mkataba wa miaka minne ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.
Nyota huyo alijiunga na United akitokea Arsenal kwa kitita cha Pauni Milioni 24 Agosti mwaka 2012 na alianza vyema msimu wake wa kwanza akimaliza kama Mfungaji Bora wa EPL wakati taji likienda Old Trafford.
Lakini Van Persie sasa amepungua makali kutokana na kuwa chini ya kiwango kutokana na majeruhi yaliyomuandama chini ya kocha Louis van Gaal.
No comments:
Post a Comment