STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 19, 2015

Beki Mtogo apewa namba ya 'gundu' Jangwani

BEKI mpya wa Yanga kutoka Togo, Vincent Bossou ameichagua jezi yenye namba inayodaiwa kuwa na 'gundu' klabuni hapo, iliyowahi kumtesa mapro wengine waliowahi kuichezea timu hiyo hivi karibuni.
Mastraika Gelinson Santos 'Jaja' kutoka Brazil na Kpah Sherman wa Liberia waliwahi kuivaa jezi namba 9 na kupata wakati mgumu Jangwani, kiasi Mliberia kutaka maombi ya kichungaji kurejesha makali.
Hata hivyo Bossou ambaye alianza kuichezea Yanga juzi Jumapili katika pambano lao dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya amesisitiza jezi hiyo namba 9 ndiyo chaguo lake.
"Napenda kuvaa jezi namba tisa, popote ninapoenda kucheza hupenda kuitumia hjata kwenye timu ya taifa, licha ya kwamba mimi ni beki, navaa jezi yenye namba hiyo na hapa Yanga vivyo hivyo," Beki huyo alinukuliwa, huku akiwataka Wanayanga kumpa muda kuzoea mazingira na kuwapa burudani.
Kauli ya Bossou ilikuja baada ya kutokung'ara vema katika pambano hilo la Mbeya ambalo Yanga ilishinda mabao 3-2, huku dakika 45 alizocheza akishirikiana na Kelvin Yondani kabla ya kutolewa kipindi cha pili Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Jaja alishindwa kung'ara Yanga na jezi namba 9 na kutimuliwa baada ya mechi chache tu, huku Sherman alihenyeka na namba hiyo mpaka kuhitaji maombi kabla ya kutulia na kufanya yake akimaliza msimu uliopita na mabao manne na katika Kombe la Kagame alivalia jezi namba 10 iliyokuwa ikitumiwa na Jerry Tegete.
Kwa sasa Mliberia huyo yupo Afrika Kusini akicheza soka la kulipwa baada ya kuuzwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment