STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 21, 2015

Straika Msenegal atua Msimbazi, amtia tumbo joto Kiiza

Niang mwenye kofia akiwasili
Niang akipokea simu mara baada ya kuwasili kwenye hoteli aliyofikia jijini Dar es Salaam
Akiwaskiliana alipowasilia hotelin
KLABU ya Simba imezidi kujiimarisha baada ya mchana huu kumpokea straika kutoka Senegal, Papa Niang, ambaye anatarajiwa kupimwa Jumatatu wakati Simba ikiumana na Mwadui Shinyanga kabla ya kusainishwa mkataba wa kukipiga Msimbazi.
Niang ambaye ni mdogo wa nyota Mamadou Niang, mshambuliaji ambaye itachukua muda Watanzania kumsahau baada ya kuizamisha Taifa Stars kwa mabao 4 ametua akiambatana na meneja wake, Massouka Ekoko.
Ujio wa straika hutyo aliyekuwa akicheza soka la kulipwa El Salvador kunamaanisha kuwa kama mipango itaenda sawa basi kuna uwezakano wa dili la Mrundi Kevin Ndatisenga aliyeifungia Simba moja ya mabao mawili wakati wakiiua URA ya Uganda likafa.
Pia hata kibarua cha Hamis Kiiza 'Diego' ambaye ameanza kuwekewa zengwe huenda nacho kikaota nyasi, ili kutimiza idadi ya wachezaji saba wa kimataifa wanaohitajiwa na timu hiyo.
Mpaka sasa ina wachezaji sita wa kigeni ambao ni Justice Majabvi, Emiry Nibomana, Hamis Kiiza, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma, huku pia ikiwa imetoa kwa mkopo Raphael Kiongera aliyepo KCB ya Kenya.
Wakati Niang akitua leo zipo taarifa kutoka Msimbazi kwamba straika mwingine mkali atatua siku yoyote kuanzia leo kumaliza na mabosi wa Simba, ikiwa ni mikakati ya kuimarisha kikosi hicho ambacho kwa misimu mitatu hakijaonja ladha ya ubingwa wa Tanzania Bara.

Dondoo kuhusu Niang
Jina kamili: Papa Niang
Tarehe ya kuzaliwa: 5 Disemba, 1988 (miaka 26)
Mahali alipozaliwa: Matam Senegal
Urefu: Mita 1.81 
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Klabu alizowahi kuzitumikia:
Kwasasa: Mchezaji huru
2005-2006: ASC Thies 
2007: FC OPA
2008: AC Oulu
2009-2012: FF Jaro
2013: FC Vostok
2013-2014: Al -Shabab SC
2014-2015: FC Mounana

No comments:

Post a Comment