*YANGA, MTIBWA HAOO NUSU FAINALI
AZAM aibu tupu! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mabingwa hao wa Kombe la Kagame kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1 na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa kundi B.Kipigo hicho kilichopatikana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar imeifanya Azam kumaliza ikishika mkia wa kundi hilo na kuziacha Yanga na Mtibwa zitakazocheza usiku wa leo zikitinga nusu fainali kilaini na kusubiri tu kujua ipi itakuwa ya kwanza na nyingine ya pili.
Mafunzo ambayo haikupewa nafasi yoyote kwenye michuano hiyio na hasa kundi hilo la kifo, imeshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu, ingawa nayo imeaga michuano hiyo ya mwaka 2016.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Kipre Tchetche katika dakika ya 21 kabla ya Mafunzo kurejesha bao hilo dakika ya 35 Rashid Abdallah na kufanya hadi mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji, lakini hakukuwa na jipya mpaka kwenye dakika ya majeruhi wakati mpira wa faulo wa Sadick Rajabu ulipotinga wavuni ukimuacha kipa mkongwe, Ivo Mapunda akiwa hana la kufanya langoni mwake.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Azam kwa msimu huu, kwani ilikuwa haijafungwa katika mechi zake 13 za Ligi Kuu Bara na hata kwenye michuano hiyo ya Mapinduzi kwani ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa na Yanga.
Msimamo
Kundi A
P W D L F A Pts
Simba 2 1 1 0 3 2 4
JKU 2 1 0 1 4 3 3
URA 2 1 0 1 3 2 3
Jamhuri 2 0 1 1 2 5 1
Kundi B
P W D L F A Pts
Yanga 2 1 1 0 4 1 4
Mtibwa 2 1 1 0 2 1 4
Mafunzo 3 1 0 2 2 5 3
Azam 3 0 2 1 3 4 2
Wafungaji:
2-Donald Ngoma (Yanga)
Awadh Juma (Simba)
Villa Oromuchan (URA)
Mohammed Abdallah (JKU)
Kipre Tchetche (Azam)
1-Paul Nonga (Yanga)
Hussein Javu (Mtibwa)
John Bocco (Azam)
Oscar Aggaba (URA)
Emmanuel Martin (JKU)
Said Bahanuzi (Mtibwa)
Vincent Bossou (Yanga)
Mwalimu Khalfan (Jamhuri)
Ammy Bangaseka (Jamhuri)
Nassor Juma (JKU)
Ibrahim Ajib (Simba)
Rashid Abdallah (Mafunzo)
Sadick Rajabu (Mafunzo)
No comments:
Post a Comment