KOCHA
Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles
Boniface Mkwasa, amemtangaza mshambuliaji Mbwana Ally Samatta kuwa
Nahodha mpya wa timu hiyo, akichukua nafasi ya Nadir Haroub Ali
‘Cannavaro’.
Akizungumza
na leo, Mkwasa amesema kwamba uamuzi huo
umetokana na kazi nzuri ya Samatta kuitangaza Tanzania na Taifa Stars
kimataifa.
“Anastahili
kuwa Nahodha wa Taifa Stars kuanzia sasa, na ingawa tumekuwa na Nahodha
ambaye anastahili kuendelea, lakini tumeona kitu pekee cha kumlipa
Samatta kwa sasa ni beji ya Unahodha,”amesema Mkwasa.
Mkwasa
amesema kuanzia sasa Cannavaro atakuwa Nahodha wa kikosi cha wachezaji
wanaocheza nyumbani kwa ajili ya michuano ya CHAN, wakati John Bocco
atakuwa Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars chini ya Samatta.
Samatta
ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika katika sherehe
zilizofanyika usiku wa Alhamisi ukumbi wa mikutano wa Kimataifa mjini
Abuja.
Samatta
alipata pointi 127, mbele ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe, kipa
Robert Muteba Kidiaba wa DRC, aliyepata pointi 88, wakati mshambuliaji
wa Etoile du Sahel ya Tunisia na timu ya taifa ya Algeria, Baghdad
Bounedjah amepata pointi 63.
Mafanikio
ya Samatta anayeweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa ukanda w
Afrika Mashariki na Kati kushinda tuzo kubwa ya Afrika, yanakuja baada
ya kuiwezesha Mazembe kutwaa taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika,
huku akiibuka mfungaji bora kwa mabao yake nane.
Aidha,
Samatta sasa ndiye anaweza kuitwa Mchezaji Bora zaidi kuwahi kutokea
Tanzania – bada ya miaka mingi ya kutokuwa na uhakika wa nani apewe sifa
hiyo.
Samatta
alijiunga na Mazembe mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa
msimu mmoja akitokea African Lyon iliyomtoa Mbagala Market, ambayo
ilimuibua Kumbagulile FC ya kwao, Mbagala.
Chanzo-Bin Zubeiry
No comments:
Post a Comment