Ibrahim Rajab 'Jeba', akichuana na Mohammed Tshabalala wa Simba jioni ya leo na Simba kulala bao 1-0 |
Bao pekee la sekunde chache kabla ya mapumziko lililofungwa na Ibraihm Rajab 'Jeba' lilitosha kuirudisha Simba jijini dar es Salaam na kuiacha Mtibwa ikitangulia fainali yao ya tano.
temesha Simba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kuifungasha virago kurudi jijini Dar es Salaam.
Katika pambano hilo la kwanza la nusu fainali lililochezwa jioni kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani humu, Simba itabidi ijilaumu kwa kutemeshwa taji.
Na kama kuna mtu ambaye atajuta kwa kung'oka kwa Simba ni kipa Peter Manyika aliyeizawadia Mtibwa bao baada ya kushindwa kudaka mpira uliiopigwa na Shiza Kichuya na kumfanya Jeba kumpoka na kufunga bao hilo.
Mtibwa sasa inasubiri kujua itacheza na nani kati ya Yanga na URA ambazo zinaendelea kuumana muda huu.
Hizo ni fainali za tano kwa Mtibwa tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2007 ikikutana na Yanga kwa mara ya kwanza mwaka huo na kufungwa.
Pia hii itakuwa fainali ya pili mfululizo ya Mtibwa baada ya mwaka jana kucheza fainali dhidi ya Simba na kufungwa kwa mikwaju ya penalti.
Pamoja na Simba kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa na hasa katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko, lakini umakini mdogo wa washambuliaji wa Msimbazi wakiongozwa na Danny Lyanga, Mussa Mgosi na Ibrahim Ajib.
No comments:
Post a Comment