STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, May 30, 2016

Ngoma? Haendi kokote, uongozi Yanga wasisitiza

Ngoma (kushoto)
TAARIFA hii huenda ikapunguza presha za mashabiki wa Yanga, baada ya uongozi wao kusema kwa herufi kubwa kuwa 'NGOMA HAENDI KOKOTE KULE'.
Uongozi wa Yanga umetoa kauli hiyo kukanusha taarifa zilizoenea mtaani kuwa, straika wao mkali, Donald Ngoma anataka kuihama klabu hiyo.
Kuna taarifa ambazo zimesambaa kupitia baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zikidai nyota huyo kutoka Zimbabwe aliyefunga mabao 17 katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, alikuwa mbioni kutimkia Afrika Kusini na Misri ambao kuna klabu zinamnyemelea wakati mkataba wake ukiwa umesaliwa na mwaka mmoja kabla ya kuisha.
"Klabu ya bado ina mkataba wa mwaka mmoja na Ngoma baada ya kumalizika kwa msimu huu. Bado hatujapokea ofa kutoka klabu yoyote inayomtaka. Hizo ni taarifa ambazo siyo rasmi na wanachama na mashabiki wanatakiwa kuzipuuza," Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alisema mchana huu.“Ngoma anaipenda Yanga na anafurahia maisha ya Tanzania. Ameshaanza kujifunza Kiswahili na kama mwenzake Kamusoko ambaye tayari anazungumza vizuri Kiswahili, na inaashiria ni kwa kiasi gani anafurahia kuwa hapa”, amesisitiza Muro.
Yanga ilimnyakua Ngoma katikati ya mwaka jana kutoka FC Platinum baada ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho ambapo Yanga iliing'oa timu yake kwa mabao 5-2.

No comments:

Post a Comment