STRIKA
USILIKOSE
Monday, June 10, 2013
MAGDALENA OLOTU AWA REDD'S MISS KIGAMBONI 2013
Mengi awaonya wanaowania Urais 2015
MWENYEKITI wa makampuni ya IPP Reginald Mengi ametoa ya moyoni kwa wote wenye mpango wa
kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka miwili ijayo.
Mengi
ameyatoa maombi yake ya m
oyoni na kuyaweka hadharani kupitia akaunti yake ya
twitter June 7, na hiki ndicho alichokiandika.
“Nawaombea
Mungu wanaotaka Urais wasipokee mshiko wa mfanyabiashara fisadi mkubwa ambaye
pia ni kinara wa madawa ya kulevya.”
Chanzo: Upekuzi Huru
Washindi wa tuzo za Kili Music Awards 2013 hawa hapa
![]() |
![]() |
| Add caption |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
![]() |
KIKUNDI BORA CHA TAARABU-JAHAZI MODERN TAARAB
MTUNZI BORA WA TAARABU-THABIT ABDUL
WIMBO BORA WA TAARABU;KHADIJA KOPA-MJINI CHUO KIKUU
MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA KWA TAARABU-ENRICO
MSANII BORA WA KIKE -TAARBU; ISHA MASHAUZI
MSANII BORA WA KIUME -TAARABU; MZEE YUSUPH
WIMBO WENYE VIONJO VYA ASILI-MRISHO MPOTO ft DITTO-CHOCHEENI KUNI
MTUNZI BORA WA MASHAHIRI BONGO FLAVA-BEN POL
MTAYARISHAJI BORA WA MWAKA-MUZIKI WA KIZAZI KIPYA; MAN WALTER
MSANII BORA WA KIUME BONGO FLAVA-DIAMOND
MSANII BORA WA KIKE BONGO FLAVA-RECHO
MTUNZI BORA WA MASHAHIRI HIP HOP-KALA JEREMIAH
WIMBO BORA WA BONGO POP;OMMY DIMPOZ-ME AND YOU
MSANII BORA ANAYECHIPUKIA-ALLY NIPISHE
MSANII BORA WA KIUME-DIAMOND
KIKUNDI BORA CHA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA-JAMBO SQUAD
MTAYARISHAJI CHIPUKIZI WA MWAKA-MENSEN SELECTA
WIMBO BORA WA BENDI;MASHUJAA-RISASI KIDOLE
MTUNZI BORA WA MASHAHIRI -BENDI; CHARLS BABA
MTAYARISHAJI WA WIMBO WA MWAKA-BENDI ;AMOROSSO
MSANII BORA WA KIKE-BENDI ;LUIZA MBUTU
MSANII BORA WA KIUME-BENDI ;CHARLS BABA
BENDI BORA YA MWAKA-MASHUJAA BAND

WIMBO BORA WA ZOUK; AMINI -NI WEWE
WIMBO BORA WA REGGAE;WARRIORS FROM THE EAST-KILIMANJARO
WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL; DABO-PREDATOR
MSANII BORA WA HIP HOP-KALA JEREMIAH

WIMBO BORA WA HIP HOP; NAY WA MITEGO-NASEMA NAO

WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI;JOSE CHAMELEONE-VALUVALU

WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA;OMMY DIMPOZ ft VANESSA-ME AND YOU
WIMBO BORA WA MWAKA; KALA JEREMIAH-DEAR GOD
VIDEO BORA YA MWAKA;OMMY DIMPOZ-BAADAE
HALL OF FAME-KILIMANJARO BAND WANA NJENJE

HALL OF FAME-SALUM ABDALLAH YAZIDU

MSANII BORA WA KIKE-LADY JAY DEE
![]() |
KASEBA ALIVYOMSAMBARATISHA SIMWANZA WA MALAWI
| Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akioneshana kazi na
JOSEPHER NJELEKELA(KAMANDA WA KAMANDA) wakati wa mpambano wao Maokola alishinda kwa KO ya raundi ya tatu
|
| Bondia Juma Fundi akioneshana umwamba na Moro Best wakati wa mpambano huo |
|
| Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
| Bondia Japhet Kaseba kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Rasco Simwanza wa Malawi wakati wa mpambano wao wa Ubingwa wa Kimataifa wa PST mpambano uliofanyika Dar es salaam jana Kaseba alishinda kwa TKO ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
| Bondia Rasco Simwanza kutoka Malawi kushoto akipambana na Japhet Kaseba wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Kimataifa wa PST kaseba alishinda raundi ya tano |
| Bondia Japhet Kaseba akiwa amevishwa mkanda wake wa kimataifa wa PST |
| Bondia Kaseba akishangilia ushindi zaidi tembelea www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Watanzania wang'ara katika mbio nchini Kenya
KATIKA kuhakikisha riadha nchini Tanzania inafuta uteja kwa wakimbiaji
wake kwa wafukuza upepo wa Kenya, Klabu ya Holili (HYAC) ya Mkoani
Kilimanjaro imedhihirisha hilo katika Taveta Athletics Championship
kwa kuwabwaga Wakenya katika mbio za meta 5000, 1500, 800 na 100.
Michuano hiyo ya Taveta imefanyika mwishoni mwa wiki katika Kaunti ya
Taita-Taveta katika Mkoa wa Pwani nchini Kenya katika wilaya ya Taveta
kwa kuwakutanisha wanariadha wa nchini Kenya huku Holili Youth
Athletics Club ikialikwa kutoka nchini Tanzania.
Katika Mbio za meta 5,000 alikuwa ni Baraka Williams aliyekimbia kwa
dakika 14:45:22 nafasi ya pili ikishikwa na Mtanzania mwingine
Abubakar Joel aliyekimbia kwa muda wa 16:00:00 na nafasi ya tatu
ikashikwa na Mkenya Kivoko Makao ambaye alikimbia kwa muda wa
16:34:00.
Wambura Lameck, Mtanzania kutoka katika klabu ya Riadha kwa vijana
(HYAC) alionyesha uwezo katika mbio za meta 100 na 800 kwa wanaume;
katika mbio za meta 100 Wambura alikimbia kwa muda wa sekunde 12:67
akiwatupa Wakenya Walter Kamujalo (13:12), Emmanuel Paulo (13:70) na
Joseph Daudi (14:20).
Mbio za mita 800 Wambura Lameck alikimbikia kwa muda wa dakika 2:02:16
akimwacha Mkenya Ropya Nyingi ambaye alichukua muda wa dakika 2:04::14
na nafasi ya Tatu ikishikwa na Mtanzania kutoka HYAC Paulo Jackson
aliyekimbia kwa muda wa dakika 2:05:98, Wakenya wengine Joseph Daudi
(3:00:00) na Philip Matheka (3:04) walisshika nafasi mbili za mwisho.
Pia Watanzania waliwaonyesha kazi nyingine Wakenya katika mbio za meta
1500 pale Baraka Williams kutoka HYAC alipowakimbiza na kuongoza baada
ya kumaliza kwa muda wa dakika 3:48:77 akifuatiwa na Mkenya Vicent
Daniel kutoka Taveta aliyemaliza kwa kutumia muda wa dakika 4:16:85
nafasi ya tatu ikishikwa na Mtanzania mwingine kutoka HYAC Paulo
Jackson ambaye alikimbia kwa dakika 5:04:66 na Mkenya Tumuna Ludovick
akikimbia kwa muda wa dakika 5:09:07.
Kwa upande wa wanawake Watanzania Furaha Sambeke na Pendo Pamba
walifanya kweli katika meta 800 kwa kushika nafasi mbili za juu.
Furaha Sambeke anayenolewa na Klabu ya Holili Youth Athletics
alikimbia kwa muda wa dakika 2:30:00 na Pendo Pamba akimaliza kwa
dakika 3:10, nafasi ya tatu ilishikwa na Mkenya Emily Wamboi na ya nne
ikishikwa na Mkenya mwingine Cecily Kimale ambao wote walikimbia kwa
kuda wa dakika 3:22:00 na 4:12:00.
Taveta Athletics Championship imefanyika ikiwa na makusudi ya
kutengeneza Timu ya Riadha ya Taifa la Kenya ambako mchujo rasmi
utafanyika Mjini Mombasa kwa watanzania walioshinda katika mbio hizo
nao watakuwemo katika kinyang’anyiro hicho kwa ajili ya kupata uzoefu
zaidi kutokana na ukweli kwamba taifa la Kenya limekuwa bora katika
riadha barani Afrika.
Mwandishi: Johnsona Jabir, Moshi-Kilimanjaro

Saturday, June 8, 2013
Wajasiriamali wanawake wazidi kupiga hatua Tanzania
EBU angalia matangazo ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali wa kike wa Tanzania...unadhani wakiwezesha zaidi si watafika mbali zaidi?!
![]() |
Subscribe to:
Posts (Atom)