STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 23, 2013

Mahafali ya Tano ya Kidato cha Nne Mwandege Boy's yalivyofana leo Mkuranga

Wanafunzi waliosalia shuleni wakisimama kumpokea mgeni rasmi
Hata wazazi na walezi nao walisimama wima
Pre Form One nao walikuwapo katika mahafali hayo
Wanafunzi wa kidato wa tatu wakionyesha onyesho la lugha ya Kiswahili kusherehesha mahafali hayo ya leo
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wakiwa wametulia vitini
Mwandege Boys kuna vipaji vya uigizaji usipime!
Yaani ni Full Kidigitali Mwandege Boys
Igizo likiendelea kuhusiana na umuhimu wa kuzingatia masomo shuleni
Hata Bongo Movie hawaoni ndani kwa madogo hawa, vipaji vitupu
Wahitimu wa kidato cha Nne Jesse na Godwin wakisoma taarifa ya habari hawa jamaa nouma

Hashim Abdallah (kulia) akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne

Wanafunzi wa kidato cha nne wakitumbuiza
Leo tunawaaga kwaherini tuliwazoea kaka zetu, ndivyo wanavyoimbiwa wahitimu waliokaa na wanafunzi wenzao wa kidato cha tatu
Yaani ni full burudani


Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mhe. Mercy Silla (wa pili kulia) akiwasili eneo la tukio akisindikizwa na Mkuu wa Shule, Mwl Enock Walter (kulia)


Meza kuu ikishuhudia vipaji vya wanafunzi wa Mwandege Boys Sec
Mashairi nayo yalisomwa kuwaaga wahitimu
Mmoja wa wazazi akitoa nasaha zake

Mzazi wa kiume naye alitoa nasaha zake.
Mkuu wa Shule ya Mwandege Boys, Mwl Enock Walter akisoma risala

Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sillah akisoma risala yake ambapo aliwataka wahitimu kutojiingiza kwenye kishawishi cha biashara za dawa za kulevya kwa nia ya kutaka utajiri wa haraka badala yake wakomalie kujiendeleza kimasomo na kutumia vipaji walivyonayo kujiletea mafanikio maishani mwao.
Mgeni rasmi (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwandege, Joseph Awino sehemu ya vitabu vilivyotolea na uongozi wa Shule ya Mwandege Boys kwa shule hiyo ya msingi ili kusaidia kukuza taalum

Mwanafunzi wa Pre Form One, Benard Deogratius aliyefanya vizuri katika masomo yake hayo akikabidhiwa zawadi na Mgeni rasmi

Mhitimu akikadhiwa cheti chake
 

Hata walimu nao walitunukiwa vyeti kwa kufanya vyema shuleni MwandegeBoys Sec

Mmoja ya wahitimu akikabidhiwa cheti na DC Mercy Sillah

Friday, November 22, 2013

Maguli aomba sapoti nje ndani Kili Stars ibebe Chalenji Kenya

Elias Maguli
MSHAMBULIAJI mpya na chipukizi wa timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars, Elias Maguli, amewaomba watanzania waliopo Kenya na wale wa nyumbani Tanzania kuwaunga mkono katika ushiriki wao wa michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza Jumatano nchini humo.
Maguli alisema kwa watanzania wanaobaki nyumbani waiunge mkono timu hiyo kwa kuiombea dua na kuifanyia maombi, huku wale wa wanaishi Kenya kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwashangili ili timu hiyo ifanye vyema katika michuano hiyo inayoshirikisha timu za nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza na MICHARAZO mchana huu katika mahojiano maalum, Maguli anayeichezea Ruvu Shooting na kushika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, alisema bila kuungwa mkono ni vigumu Kili Stars kufanya vyema katika michuano hiyo.
Maguli alisema wachezaji wa kikosi hicho kinachotarajiwa kuondoka Jumatatu kabla ya Alhamisi kuwavaa Chipolopolo ya Zambia wamejiandaa vya kutosha kuwapa raha watanzania kutokana na maandilizi waliyofanya chini ya kocha wao, Kim Poulsen, lakini sapoti ya mashabiki ni muhimu.
"Wachezaji tumejiandaa vya kutosha kutowaangusha watanzania, nasi tunaomba tuungwe mkono kwa wlaiopo Kenya wajitokeze uwanjani na wale wa nyumbani watuunge mkono kwa sala na maombi na hatimaye tutarejea na kikombe Mungu akipenda," alisema.
Kuhusu kuwemo kwenye kikosi hicho cha Kili Stars, Maguli alisema anajisikia fahari kwa kuwa Tanzania ina wachezaji bora na nyota lakini kocha amemuona anastahili kuiwakilisha nchi na atapigana kiume akishirikiana na wenzake ili kuipa timu hiyo taji lake la nne.
Tanzania Bara imenyakua ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1974, 1994 na 2010 na mara nyingine zote tangu michuano hiyo ianze kutambuliwa kama Chalenji miaka 40 iliyopita imekuwa kama msindikizaji tu.

Breaking Newzz: Zitto Kabwe apigwa 'stop' CHADEMA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIWLSkbykk_sjO3i9lNEUs2svxN7oCsv5Vbr-4u7kxDo_t6240fLBSEFxdQguEQHn_YHmZqr182kNLPNwkv8REW_MaB8TqVLjt_8pgK5wCwBi1YPChOby84dZbTcwqj3D90RVMlZpRUKc/s1600/chadema.jpg
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeeman Mbowe akizungumza kwenye kikao hicho (Picha:CHADEMA Blog)
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa CHADEMA kimeamua kumsimamisha na kumvua nyadhifa zote aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini na wamempa muda wa saa 78 kujieleza kwa nini asifukuzwse chamani kimoja.
MICHARAZO inafuatilia kwa kina na itawafahamisha, hii ni ikiwa ni maamuzi ya kikao cha Kamati kuu ya chama hicho kilichoanza kukutana tangu juzi.

Nyilawila awashukia mabondia wenzake wanaendekeza wanga

BONDIA Kalama Nyilawila 
BONDIA  Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani
za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi  ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema  hapendezwi na
vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini.
Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa
wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia
kufanya vema,"alisema.
Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano
lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake
jitihada zake binafsi  ulingoni ndizo zitakazomfaa.
Alisema watu wasitafute mchawi  aliyesababisha Tanzania isifanye vema
kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa
wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake
Seleman Zugo na kwamba  amejipanga kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa KO  ya raundi ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika Novemba 10 jijini Dar es Salaam.

Thursday, November 21, 2013

Simanzi tupu rufaa ya Babu Seya

MSANII JOSEPH MARA AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUTOLEWA HUKU NA KUTUPILIA MBALI
WATU MBALIMBALI PAMOJA NA JAMAA ZAO WAKICHUNGULIA KWENYE  CHUMBA CHA MAHAKAMA MARA BAADA YA KUTUPILIA MBALI KWA KUTUMIA MLANGO WA VIOO
BAADHI YA NDUGU WAKILIA WAKATI NGUZA NA  MWANAE WAKIPANDA GARI LA MAGEREZA LEO
BAADHI YA NDUGU WAKILIA WAKATI NGUZA NA  MWANAE WAKIPANDA GARI LA MAGEREZA LEO
BAADHI YA NDUGU WAKILIA WAKATI NGUZA NA  MWANAE WAKIPANDA GARI LA MAGEREZA LEO
BAADHI YA WATU MBALIMBALI WALIOFIKA KATIKA MAHAKAMA YA RUFAA LEO
NDUGU NA JAMAA WAKILIA KWA HUZUNI KATIKA MAHAKAMA HIYO LEO
BAADHI YA NDUGU WAKIMUAGA NGUZA VIKING NA MWANAE JOHNSON NGUZA 'PAPII KOCHA'
WANAMUZIKI NGUZA VIKING NA JOHNSON NGUZA 'PAPII KOCHA'  WAKIWAAGA NDUGU NA MASHABIKI NA JAMAA WALIOFIKA KWENYWE MAHAKAMA YA RUFAA LEO BAADA YA KUTUPIWA MBALI

WAKIPANDA KWENYE GARI LA MAGEREZA

WATUI MBALIMBALI PAMOJA NA JAMA WAKIMUAGA BABU SEYA WAKATI GARI LA MAGEREZA LIKONDOKA LEO MAHAKAMA YA RUFAA

WAKIPANDA KWENYE GARI LA MAGEREZA

WAKITOKA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA YA RUFAA LEO

BAADHI YA JAMAA ZAO WAKILIA HUKU WAKIWAPIGIA SIMU JAMAA ZAO LEO

Kilimanjaro Stars kwenda Kenya J'3 Kim ataja silaha 23um

Kocha Kim Poulsen
KOCHA Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Kombe la CECAFA Challenge inayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 27 mwaka huu.
Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho mwaka 2010 chini ya Kocha Jan Poulsen, na ambayo imepangwa kundi B katika michuano ya mwaka huu itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28 mwaka dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu (Novemba 25 mwaka huu) kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 mwaka huu na kumalizika Desemba 13 mwaka huu. 
Katika hatua nyingine; Mechi ya kirafiki ya kimataifa ya FIFA Date kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (The Warriors) iliyochezwa juzi (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,980,000 kutokana na watazamaji 7,952.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 7,776,610.17 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 3,682,560.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 5,928,124, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 7,904,166 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,976,041.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 17,784,373 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 889,219 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Maafisa 77 wa Jeshi la Polisi waula...Soma majina yao

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


RAISs wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 77 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Miongoni mwa maafisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Engelbert Kiondo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP. Marietha Minangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP. Diwani Athumani na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela.

Wengine ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP. Frasser Kashai, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP. Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP. David Misime, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP. Ferdinand Mtui, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP. Costantine Massawe, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP. Leornad Paul, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP. Ulrich Matei na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP. George Mwakajinga.


Zaidi ya hao wengine ni, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Evarist Mangala, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusedit Nsimeke, Kamanada wa Polisi mkoa wa Njombe ACP. Fulugence Ngonjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari na baadhi ya Makamanda wa vikosi, Wakuu wa vitengo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es salaam.


Kufuatia kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Aidha, IGP Mwema amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo, na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika kuimarisha Usalama wa raia na mali zao kwa kuwa cheo ni dhamana.



Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa jeshi la polisi