STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 2, 2013

Coastal Union mabingwa wapya Uhai Cup

 
MABAO mawili yaliyofungwa kipindi cha pili yalitosha kuiwezesha Coastal Union ya Tanga kunyakua taji la Uhai Cup ikiwa ni mara yao ya kwanza baada ya kuifunga Yanga katika pambano la Fainali la michuano hiyo.
Pambano la kuhitimisha michuano hiyo inayoshirikisha timu za vijana U20 lilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi, lilishuhudia timu hizo zikienda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Coastal kuonyesha dhamira ya kulipa kisasi cha kufungwa 2-1 na Yanga katika mechi ya makundi kwa kujipatia bao la kuongoza lililofungwa dakika ya 52 na Ally Nassor.
Dakika moja kabla ya kumalizika kwa pambano hilo, Mahadhi Juma aliongeza bao la pili kutokana na pasi za videoni zilizopigwa na wachezaji wa Coastal ndani ya lango la Yanga kabla ya mfungaji kutumbukiza wavuni.
Kwa kutwaa ubingwa huo, Coastal wamezawadiwa Sh. Milioni 2 na wadhamini wa michuano hiyo, Maji ya Uhai wakati washindi wa pili Yanga wamezawadiwa Sh. Milioni 1.5 na Azam FC walioshika nafasi ya tatu wamepewa Sh. Milioni.
Mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa Tanzania, Salum Kabunda ‘Ninja Msudan’ (sasa marehemu) aitwaye Ally Salum Kabunda wa Ashanti United ameibuka mfungaji bora wa mashindano kwa mabao yake tisa, ingawa timu yake iliishia Robo Fainali na kutolewa na Yanga.   
Azam walipata nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mtibwa katika pambano lililotangulia fainali hiyo kwa mikwaju ya penati 3-1 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 3-3.
Dakika 90 za awali timu hizo zilifungana mabao 2-2 na katika muda wa nyongeza za dakika 30 timu hizo zilifungana tena bao 1-1 na kufanya matokeo kuwa 3-3 kabla ya kupigiana penati. Azam ndiyo waliokuwa mabingwa watetezi wa taji hilo.

Tmasha la ngumi lafanya Mwenge

Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo, wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya viongozi na waau wa mchezo wa masumbwi wakifatilia mashinano hayo ya ngumi kwa ajili ya kuhamasisha tuzo za Boxing AWARD zitakazofikia kirere Desemba 28 mwaka huu wa 2013
Mabondia wa uzito wa juu Kulwa Makenzi kushoto akipambana na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya wazi ya kutangaza tuzo za Tanzania Boxing Awards ambazo kilele chake kitakuwa Desemba 28 Swanga alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hamad Furahisha kushoto akimsukumiza konde la kulia George Costantino wakati wa uzindunzi  wa Tuzo za Tanzania Boxing Awards iliyofanyika katika kituo cha mabasi mwende Dar es salaam Furahisha alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Matangazo ya kuamasisha tuzo za ngumi

mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi akibandika tanzazo la kuhamasisha masumbwi

Bondia Haruna Swanga akipiga picha kwenye bango

Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia John Christian kushoto akitupa ngumi ya kulia wakati wa mpambano wake  na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha mpya wa Azam ndiye huyu hapa!

 Kocha mpya wa Azam FC Joseph Omog akiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Ndugu Said Mohammed.

 Omog na Mwandishi wa habari za michezo,Mwani Nyangasa.
 Kocha Omog akikabidhiwa jezi ya Azam FC.





Klabu ya Azam inapenda kuufahamisha umma hususan wapenzi wa mpira wa miguu kuwa imeingia mkataba na kocha Joseph Marius Omog raia wa Cameroon kwa kipindi cha ...
miaka miwili (2) kuanzia leo.

Kocha Omog ni bingwa kwani anakuja kuifundisha Azam akiwa ametoka kuiongoza klabu ya A.C Leopards ya Jamhuri ya Kongo (Brazaville) kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013).

Timu hii ilikuwa haijatwaa ubingwa wa ligi kwa zaidi ya miaka 30. Kwa mwaka huu wametwaa ubingwa wakiwaacha wapinzani wao, Diables Noirs kwa pengo la pointi kumi (10) wakikusanya pointi 87 katika ligi yenye timu 18.


Pia ni mwaka jana tu (2012) aliiwezesha A.C Leopards kunyakua ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika kwa kuzipiga kumbo timu ngumu na zenye uzoefu mkubwa kama vile Mas de Fes ya Morocco, Heartlands ya Nigeria na Sfaxien ya Tunisia.  
Mafanikio hayo ya kutwaa ubingwa wa Afrika yalifikiwa baada ya miaka 38 tangu klabu ya Jamhuri yas Kongo ifanye hivyo, na kumfanya kocha Omog kuwa moja ya makocha wa kupigiwa mfano barani Afrika.

Kadhalika mwaka huu 2013, A.C Leopards chini ya ukufunzi wa Omog ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya mabnigwa Afrika na kupangwa katika kundi moja na timu mbili zilizocheza fainali; Al Ahly ya Misiri (bingwa) na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Yote hayo ameyafanya akitumia asilimia kubwa ya wachezaji wa ndani ya Kongo huku akiwainua kutoka katika hali ya kuonekana wachezaji wa wastani hadi kuwa tishio na kuhofiwa kote barani Afrika.

Azam Football Club inamuona kocha Omog kuwa anakidhi vigezo vya kuendana na dira ya klabu ambayo ni kukuza na kuwaendeleza wachezaji na kushindana kwa kiwango cha juu kwa lengo la kuwa mabingwa katika mashindano mabalimbali ambayo timu inashiriki.

Uongozi wa Azam FC utampatia ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo na mipango thabiti ya klabu.

Maelezo Binafsi
Kocha Omog ni mchezaji wa zamani wa timu ya Dragon Yaounde Cameroon. Alipata mafunzo ya ualimu wa michezo na elimu ya viungo (Sports and physical education) kutoka chuo cha vijana na michezo (Higher Institute of Youth and Sports, INJS Yaounde).

Baadaye alipata fursa ya kujiendeleza nchini Ujerumani ambako mwaka 1987 alitunukiwa stashahada ya ukufunzi wa mpira wa miguu na leseni B ya ukocha kwa viwango vya Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya, UEFA.

Aliporejea nyumbani kwao Cameroon Joseph Marius Omog, alifundisha kabumbu katika klabu mbalimbali, zikiwemo; Fovu of Baham na Aigle of Menoua na kufanikiwa kufuzu kwa fainali za kombe la Cameroon. Mwaka 2001 aliteuliwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon, Indomitable Lions chini ya kocha raia wa Ujerumani Winfried Schafer.

Omog amewahi pia kufundisha timu ya taifa ya Cameroon iliyoundwa na wachezaji wa ndani ijulikanayo kama Intermediate Lions hadi mwaka 2010 na baada ya hapo akelekea Kongo kuionoa A.C Leopards kwa mafanikio makubwa na hasa kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho wakiifunga Djoliba ya Mali kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-3 katika michezo miwili ya fainali.