STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Mourinho aomba radhi kwa kumuuza Mata kwa Mashetani

Mourinho akiwa na Mata enzi wakiwa pamoja Chelsea
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameomba msamaha kwa uamuzi wake wa kumuuza Juan Mata Manchester United na kuweka wazi kuwa "ulikuwa uamuzi mgumu" kumuacha kiungo huyo raia wa Hispania kujiunga na mahasimu wao hao wa Old Trafford.
Mata, 25, ameweka rekodi United ya uhamisho baada ya kujiunga nayo kwa paundi milioni 37 akitokea Chelsea, ambako alikuwa hana raha tangu kocha huyo wa kireno kutua Stanford Bridge..
Mourinho aliiambia BBC Radio 5  kuwa angelipenda kuendelea kuwa na Mata katika kikosi chake.
"Kuna uamuzi ambao kocha anatakiwa kuchukua, lakini kwangu mimi ulikuwa uamuzi mgumu. Ningependa kuwa naye katika kikosi changu," alisema Mourinho.
"Mata ni mfungaji mzuri, lakini kuwa na mchezaji katika hali kama hii ni ngumu. Alistahili hilo kwa Chelsea kumfungulia mlango [akapate nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza].
"Ninapenda watu kuwa na furaha. Naomba msamaha sikuweza kumfanya kuwa na furaha katika kikosi hiki - Nimeumia sana katika hilo, lakini ninajenga timu yangu kwa kumchezesha Oscar kama namba 10."
Pia Mourinho alisema pindi Mata atakaporejea Stamford Bridge akiwa na United atamhakikishia mapokezi mema kutoka kwa mashabiki wa Chelsea.
"Ni wa kipekee sana. Nadhani ni 'mchezaji ambaye atabaki kuwa rohoni mwa mashabiki' na pia katika kizazi hiki," aliongeza Mreno huyo.
"Nimekuwa naye kwa kipindi cha miezi sita tu na nilimpenda sana. Sasa chukulia kwa watu ambao wamekuwa naye kwa miaka mitatu. Atabaki kuwa katika historia ya klabu - ametwaa makombe muhimu na watu wanampenda.
"Siku moja atakuja hapa akiwa na jezi ya Manchester United na watu watamuonyesha upendo huo." 

Mashindano ya Ngumi Ilala yaanza

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindan ya  wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point 
Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es salaam DABA akimkabidhi risara Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu wakati wa mashindano ya wazi yaliyoanza jumatatu

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kulia  akimtupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point
 Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akifatilia mchezo wa ngumi
Na Mwandishi Wetu

SHILIKISHO la ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tanga waingie Madarakani mashindano hayo yalifunguliwa jumatatu na mgeni rasmi


Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ambayo imekutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huu akisoma risala kwa mgeni rasmi 


Mwenyekiti wa ngumi mkoa wa Dar, Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changamoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye karenda yao ata hivyo akuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la ilala tunaomba utupatie angarau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo avikizi kimchezo


akijibu risara hiyo mbunge huyo ame haidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele 


katika ufunguzi huo mabondia Anton Idoa alimtwanga kwa K,O ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said, na shabani Alimasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya shanti ya Ilala,Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi na Ayubu Ibrahimu  

Monday, January 27, 2014

Huzuni! Muigizaji huyu wa Futuhi afariki dunia




HABARI zilizotufikia zinasema muigizaji, Mzee Dude amefariki dunia leo jioni baada ya jana kupatwa ghafla na maradhi na kukimbizwa hospitalini.

Man City vs Chelsea, Arsenal vs Liverpool FA Cup



DROO ya Raundi ya 5 ya FA CUP imefanyika leo ambapo bahati imezikutanisha vigogo vilivyopo kwenye Top 5 ya Ligi ya England, ambapo Manchester City itaavana na Chelsea na Arsenal itakutana na  Liverpool.
Mechi zingine zitakazohusisha timu za Ligi Kuu ya England ni kati ya Sunderland v Southampton na Everton v Swansea.
Mechi hizi zitachezwa wikiendi ya Februari 15 na 16 na Washindi kutinga Robo Fainali.
Droo hiyo ilifanyika huko Wembley Stadium Jijini London na kuendeshwa na Andros Townsend, Mchezaji Chipukizi wa Tottenham, pamoja na Baba yake Mzazi, Troy, ambae ni Mwanaharakati maarufu kwenye Soka.
RATIBA KAMILI:
Manchester City v Chelsea
Sheffield United AU Fulham v Nottingham Forest AUr Preston NE
Arsenal v Liverpool
Brighton v Hull
Cardiff City v Wigan
Sheffield Wednesday v Charlton
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea

Simba, Yanga zaingiza Mil 139

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjIcondyKwoFCu6HZwULhEbB0KogLLWJzzr8fQ-G3EXLUiql5BUq8DuVwMHQTPxQBQs-fIgqEWxFG11jAd3BpggLzNc3a1e1Uj25TLwKl4zksNZE5EuSQTATHsdycqlpMe4-v2tMSksPTb0/s1600/DSC_0616.JPG
Na Boniface Wambura
MECHI za Ligi Kuu ya Vodacom zilizohusisha timu za Simba na Yanga na kuchezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiendi zimeingiza jumla ya sh. 139,850,000.
Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake liliingiza sh. 86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza sh. 53,815,00 kwa watazamaji 9,629.
Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 13,123,983.05, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 20,650,211.50.
Uwanja sh. 10,500,107.54, gharama za mechi sh. 6,300,064.53, Bodi ya Ligi sh. 6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,450,025.09.
Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,910,300 wakati kila klabu ilipata sh. 12,595,211.50.
Uwanja sh. 6,404,344.83, gharama za mechi sh. 3,842,606.90, Bodi ya Ligi sh. 3,842,606.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,494,347.13.
Vilevile tiketi zinapatikana kupitia maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo katika maeneo mbalimbali nchini. Watakaonunua kupitia maduka hayo watapata tiketi na kwenda moja kwa moja uwanjani.
Wakati huo huo: Mauzo ya tiketi za elektroniki kwa mechi tatu kati ya nne za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa keshokutwa (Januari 27 mwaka huu) tayari yameanza, hivyo wanatakiwa kununua mapema.
Mechi hizo ni kati ya Coastal Union na Yanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na ile ya Azam dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kwa washabiki wa Dar es Salaam watakaokwenda Tanga kushuhudia mechi kati ya Coastal Union na Yanga wanashauriwa kuanza safari wakiwa na tiketi zao mikononi, hasa kwa wale watakaonunua kupitia maduka ya Fahari Huduma.
Tiketi pia zinaweza kununuliwa kupitia mtandao wa M-Pesa kwa kupiga namba *150*03*02#. Kwa wanaotumia CRDB simbanking wanaingia kawaida kwa *150*03.
Vilevile tunawakumbusha washabiki kuwa kwa viwanja ambavyo tayari vina mfumo wa tiketi za elektroniki hakuna tiketi zitakazouzwa uwanjani, hivyo wanaokwenda kwenye mechi wanatakiwa kuwa na tiketi zao mikononi.