STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 13, 2014

Yazidu apigwa KO, Alibaba atwaa ubingwa wa UBO-Africa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCFv47mCVl3aUXjxh6a6KtndNnR4Bp8jHfeYNutiWBvVwfEra6dqdkHcbwQEuG1SBFWDBVQ0RvCQYOnLM5r2rrVkah2pShawIEfGNsiWCffTIIS5K4yvb8X65OP0Gd4EZDHTRu6QY5QOoJ/s1600/IMG_0862.JPG
Bondia Djamel Dahou wa Algeria aliyempiga Yazidu kwa KO ya raundi ya kwanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjw4HnzsBYYU8jB2t_dJEgfckbaym7OawUnrumIA9LSQgWb7iHKdEWHQ3xRKMCQQ705e-I4nMn8GL-hBJjDLBpSa4almGOJg0yPfi9iNrX9Es0rcsuSqjwkJ-hPVO9ech5hZ74PKlSn7us/s1600/DSCF1317.JPG
Alibaba (kulia) akatika mazoezi kabla ya kushinda jana dhidi ya Mmalawi
BONDIA Said Yazidu ameshindwa kutamba nyumbani baada ya kupigwa kwa KO ya raundi ya kwanza na Djamel Dahou kutoka Algeria katika pambano la kuwania Ubingwa wa Dunia wa UBO, lililofanyika usiku wa jana kwenye ukumbi wa YMCA, Moshi Kilimanjaro.
Hata hivyo watanzania walijifariji baada ya bondia Ali Ramadhani 'Alibaba' kumshinda kwa pointi Mmalawi Alick Mwenda na kutwaa mkanda wa UBO Afrika katika pambano jingine la kimataifa.
Yazidi mmoja wa mabondia wakongwe waliowahi kujijengea jina siku za nyuma, alishindwa kuhimili vishindo vya mpinzani wake na kujikuta akishindwa kumaliza raundi ya kwanza kwa kuchakazwa na Dahou.
Mtanzania huyo alijikuta akisalimu amri kwa mpinzani wake katika dakika ya pili sekunde ya saba na kuuacha mkanda huo wa Dunia ukiondoka katika ardhi ya Tanzania.
Kabla ya pambano hilo lililokuwa la raundi 12, Ali Ramadhani maarufu kama Alibaba wa Tanzania aliweza kupambana vilivyo na kumshinda mpinzani wake kutoka Malawi, Alick Mwenda kwa pointi 100-99 katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika unaotambuliwa na UBO.
Katika pambano hilo la raundi 10 mabondia wote walionyesha ujuzi wao kwa kutupiana makonde kiufundi na ndipo majaji walipotoa matokeo yaliyompa Alibaba ushindi huo wa pointi dhidi ya Mmalawi.
Michezo hiyo na minmgine ya utangulizi iliandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).

TFF kutoa mafunzo ya Tiketi za Elektroniki

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/Wambura1.jpg
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jumamosi kuanzia saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura, mafunzo hayo Uwanja wa Taifa, yatashirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Azam na Yanga.
Washiriki wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. Tiketi zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.

Jennifer Mgendi amrudia Shelina

http://www.jennifermgendi.com/images/gallery/1361182868.jpg

MUIMBAJI nyota wa muziki wa Injili, Jennifer Mgendi amesema ataingia mzigoni kutengeneza filamu yake mpya iitwayo 'Shelina' baada ya awali kuisitisha kupisha kazi nyingine anayojiandaa kuitoa hadharani.
Jennifer alipanga kuitengeneza filamu hiyo ya Shelina mapema mwaka huu, lakini aliahirisha ili kurekodia 'Mama Mkwe' ambayo imeshakamilika na itaachiwa wiki ijayo.
Akizungumza na MICHARAZO, alisema hakuona kama ni busara kuzitengeneza filamu hizo mbili kwa wakati mmoja, ndiyo maana ataisitisha 'Shelina' ili kuimalizia 'Mama Mkwe' na baada ya hapo ndipo akirudie 'kiporo' chake ambacho atawashirikisha wasanii mbalimbali nyota wa muziki wa Injili na wale wa Bongo Movie.
Miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kushiriki filamu hiyo kwa mujibu wa Jennifer ni; Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Christina Matai na Bi Esther.
"Nilisitisha kuendelea na Shelina ili kupisha filamu ya 'Mama Mkwe' ambayo nitaiachia Sept 22, baada ya hapo kazi itaanza mara moja," alisema.
Jennifer Mgendi anayetamba na albamu kadhaa za nyimbo za Injili ikiwamo ya 'Hongera Yesu' iliyopo sokoni kwa sasa, amewahi kukimbiza na filamu kama 'Joto la Roho', 'Pigo la Faraja', 'Teke la Mama' na 'Chai ya Moto'.

Van Gaal afichua siri ya kumuuza Welbeck kwa Arsenal

Danny Welbeck
Danny Welbeck
WAKATI nyota wa zamani wa Manchester United na hata mashabiki wakishindwa kuamini kama Kocha Luis Van Gaal amemuuza Danny WElbeck kwa mahasimu wao Arsenal, meneja huyo amefichua siri ya kumtema mshambuliaji huyo.
Van Gaal amesema Welbeck aliachwa kwa sababu hakufunga mabao ya kutosha huku akidai kuwa atawapa nafasi wachezaji ndani. 
Akiongeza wakati wa kuwatambulisha wachezaji wawili waliosajili mwishoni Radamel Falcao na Daley Blind, Van Gaal alifafanua kwanini Welbeck, 23 aliuzwa kwa Arsenal kwa kitita cha paundi milioni 16. 
Van Gaal amesema Welbeck amecheza misimu mitatu akiwa na kikosi cha kwanza lakini hajafikia rekodi ya Robin van Persie au Wayne Rooney katika ufungaji. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa hiyo ndio sababu iliyomfanya auzwe kwasababu ya Falcao na pia kutoa nafasi kwa wachezaji chipukizi nao kupata nafasi.
Tangu Welbeck auzwe nyota wa zamani wa Old Trafford akiwamo David Beckham wamekuwa wakilaumu kitendo hicho kwa kuamini kuwa mshambuliaji huyo bado alistahili kubakishwa kwa Mashetani Wekundu hao kwa umahiri wake.

Diego Costa, kocha wa Swansea City funika bovu England

Diego Costa akiwa na tuzo yake
Kocha wa Swansea, Garry Monk akiwa na tuzo yake ya Mwezi Agosti
STRIKA mpya wa Chelsea, Diego Costa ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya England, huku kocha wa Swansea Garry Monk akiinyakua tuzo kama hiyo kwa upande wa makocha.
Mpachika mabao huyo aliyetokea Atletico Madrid aliyefunga mabao manne katika mechi tatu walizocheza Chelsea ameianza ligi hiyo kwa mguu wa bahati.
Wakati Costa akiing'ara hivyo, kwa upande wa  Garry Monk, Kocha wa Swansea aliwafunika makocha wenzake kadhaa baada ya kushinda tuzo ya mwezi Agosti.
Kocha huyo ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi huo baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi zake zote tatu, ikiwemo dhidi ya Manchester United Uwanja wa Old Trafford. 

Friday, September 12, 2014

Simba yalala kwa URA, kesho kuwafuata Ndanda FC

Amri Kiemba akijaribu kuwatoka wachezaji wa URA huku Emmanuel Okwi akiwa tayari kutoa msaada
KLABU ya soka ya Simba imeendeleza uteja wake mbele ya URA ya Uganda baada ya jioni ya leo kunyukwa bao 1-0 katika pambano la kirafiki la kimataifa lililochezwa kwenye uwanja wa Taifa.
Simba iliyotoka kuionea Gor Mahia kwa kuilaza mabao 3-0 ilishindwa kupata dawa ya kugeuzwa mteja wa kudumu kwa Watoza Ushuru hao wa Uganda kwa kulazwa bao hilo ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Simba kupoteza chini ya kocha Patrick Phiri.
Bao pekee lililoizamisha vijana wa Msimbazi ambayo haijaifunga URA katika mchezo wowote wanaokutana nao iwe kwenye mashindano au mechi za kirafiki liliwekwa kimiani na Frank Kalanda katika dakika ya 42, akimalizia kazi nzuri ya Elkanda Nkungwa.
Kesho asubuhi Simba itapaa angani kuelekea Mtwara tayari kwa pambano lao jingine dhidi ya Ndanda Fc katika kunogesha Siku ya Ndanda (Ndanda Day) linalofanyika kesho kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini humo.

Wahitimu Shule ya Brian Trust, wengine watahadharishwa

Mgeni rasmi wa mahafali ya Shule ya Brain Trust, Richard Mngomo alitoa nasaha zake jioni ya leo
Wahitimu wakionyesha umahiri wao wa kuimba ngonjera
Wahitimu wakielekea eneo la shughuli ya kuagwa kwao kwa kuhitimu darasa la saba
Mkuu wa Shule ya Msingi, Nervin Marandu akitoa natoa nasaha zake
Wahitimu wakiingia uwanjani kuonyesha umahiri wao
Wakiimba
Samuel Robert akiwaongoza wahitimu wenzake kuonyesha umahiri wa kuimba ngonjera
Skauti wakionyesha umahiri wao mbele ya meza kuu
Mericiana Ronald akianza kuonyesha umahiri wake wa kucheza muziki
Acha kama Aisha Madinda! Mericiana akiendelea kuangusha rhumba
Mkuu wa Shule ya Msingi, Nervin Marandu akisoma wasifu wa shule hiyo katika mahafali hayo pembeni yake ni mmoja wa walimu wa shule ya Brain Trust
Immaculatha Justine Limonga akipokea cheti chake cha kuhitimu Darasa la Saba toka kwa mgeni rasmi
WAHITIMU wa darasa la saba wa Shule za Msingi nchini kote wamehimizwa kuwa makini wanaporudi mtaani kusubiri matokeo yao ya mitihani ili kuepuka kuharibikiwa na kutumbukia kwenye maovu.
Aidha wazazi wamesisitizwa kuhakikisha wanapambana na kusaidia kuwaendeleza watoto wao kwa masomo ya sekondari badala ya kuridhika na Elimu ya Msingi wanaomaliza watoto wao.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Shule ya Brain Trust, Irene Makinda wakati wa mahafari ya wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo yaliyofanyika jioni ya leo.
Makinda alisema wahitimu wa darasa la saba wanachangamoto kubwa katika kipindi chao cha kusubiri matokeo ya mitihani yao kwani wanakutana na na makundi ya watu tofauti, hivyo wawe makini.
Alisema ni vyema wazazi wakawaunganisha watoto wao na masomo maalum ya kujiandaa kujiunga sekondari (Pre form One) ili kuendeleza kuzifanya akili zao zichemke na kuepushiwa kuingia kwenye maovu.
"Hapa shuleni tunapokea wanafunzi kwa masomo hayo hivyo wazazi wasizembee wawalete watoto na pia shule yetu ina masomo ya sekondari hivyo wanafunzi wanaweza kuendelea hapa hapa," alisema.
Naye mgeni rasmi wa sherehe hizo zilizofanyika Yombo Vituka, Richard Mgomo wa Tanzania Printers, alisema wahitimu hao wa la saba wasidhani wameshamaliza kazi badala yake wajipange zaidi kimasomo.
"Kazi haijaisha, miaka saba mmepambana na kufanikiwa kufika mlipofikia, tunawapongeza, lakini kazi haijaisha kuna mtihani mkubwa zaidi mbeleni hivyo mjipange. Msiwangushe wazazi na walezi," alisema.
Mgomo, alisema ni wajibu wa wazazi na walezi kuwaendeleza watoto wao kwa masomo ya sekondari na nafasi hizo zikipatikana wanafunzi hao wasiwaangushe wazazi na walezi badala yake wajibidiishe zaidi.
Kabla ya mgeni rasmi huyo kuzungumza, Mkuu wa Shule ya Msingi Nervin Marandu alisoma historia fupi ya shule hiyo na kusema ilianzishwa Sept Mosi, 1998 ikiwa na wanafunzi 48 tu.
Hata hivyo alisema mpaka sasa shule hiyo ya msingi ina wanafunzi wapatao 850 na kusisitiza shule yao haibagui wanafunzi wa kuwapokea na kujivunia mafanikio inayopata kila mwaka tangu ianzishwe.
Katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo walimu wa shule za jirani na wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo kulipambwa na burudani toka kwa wanafunzi.
Miongoni mwa burudani hiyo ni mwanafunzi wa shule ya chekechea ya shule hiyo ya Brain Trush Mericiana Ronald aliyeonyesha kipaji cha kucheza muziki na kutuzwa maelfu ya fedha na waliokunwa naye.

Rodgers awaka majeruhi ya Sturridge

http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/02579/daniel-sturridge_2579270b.jpgMENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema kuwa majeruhi ya Daniel Sturridge yangeweza kuepukika na Chama cha Soka cha Uingereza kinapaswa kuwaepusha wachezaji na majeruhi pindi wawapo katika majukumu ya kimataifa. 
Mshambuliaji huyo alicheza kwa dakika 89 wakati Uingereza ikishinda bao 1-0 dhidi ya Norway katika Uwanja wa Wembley Jumatano iliyopita kabla ya kurejea tena mazoezini saa 36 baadae na kupata majeruhi akiwa mazoezini. 
Sturridge, 25 alikosa mchezo ambao Uingereza iliibugiza mabao 2-0 Uswisi katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya Jumatatu kutokana na majeruhi hayo na sasa anatarajiwa kukaa nje kwa wiki mbili zaidi. 
Rodgers amesema wamesikitishwa sana kutokana kazi kubwa aliyofanya wakati wa maandalizi ya msimu kwani wanadhani majeruhi aliyopata yalikuwa yanaepukika kama wahusika wangekuwa makini. 
Liverpool itajitupa uwanjani Jumamosi hii kukwaana na Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu.

Pele asema Messi ananafasi ya kutwaa Kombe la Dunia

http://i.lidovky.cz/10/042/lnc460/ANT326be7_pele_messi.jpg
GWIJI wa soka wa Brazil, Pele amesema kwamba Lionel Messi bado anayo nafasi ya kutwaa Kombe la Dunia na kuongeza kwamba nyota huyo wa Barcelona tayari ni mmoja wa magwiji wa soka hata kama atashindwa kuiongoza Argentina kutwaa taji hilo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikaribia kubeba Kombe la Dunia wakati alipoiongoza Argentina kufika fainali nchini Brazili, lakini likatua kwa Ujerumani walioshinda katika muda za ziada.
Licha ya hivyo, Pele ameweka wazi kwamba Messi bado anayo nafasi na anaamini kwamba atapata fursa nyingine ya kutwaa tajihilo 2018.
"Hakika, Messi bado anaweza kutwaa Kombe la Dunia," Pele aliiambia DPA.
"Messi ni mchezaji aliyekamilika na yuko katika hali nzuri sana kimwili. Sina shaka kwamba bado atatamba kwenye Kombe la Dunia.
"Kufungwa katika fainali Brazil hakumuondolei ukweli kwamba Messi ni mchezaji mkubwa sana. Atapata fursa nyingine ya kutamba nchini Russia.
"Hakuna shaka kwamba Messi ni bonge la mchezaji. Hatuwezi kuhoji uwezo wake kwa sababu tu hajatwaa Kombe la Dunia bado."
Messi amecheza mechi 93 za timu yake ya taifa na ameifungia magoli 42.

Kaole Kwanza waanza mazoezi ya Kipusa

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGO1SXfSXqu1qK74H1G9dDqrWDCvkTVNk5T7hq4iyRVPXXngHa5sH7RtZYh62pFiupbwxnCH9w3zgTd5jap6z8OBuU2289az27NUf-V4mONXfcKITG0_B_EBnjRC3Bj3bs6ICLNLtYtYt3/s1600/Kaole1.jpg
Kundi la Kaole Kwanza katika picha ya pamoja siku walipozindua Kipusa chao
KUNDI la Kaole Kwanza ambalo linaoundwa na wasanii waliowahi kutamba na Kaole Sanaa, limeanza tena mazoezi kwa ajili ya kuendelea kurekodi tamthilia yao iitwayo 'Kipusa' ambayo inatarajiwa kuanza kurushwa hewani kupitia runinga.
Akizungumza na MICHARAZO mmoja wa viongozi wa Kaole Kwanza, Issa Kipemba alisema baada ya kusitishwa kwa kambi ya mazoezi ili kurekebisha mchakato wa kusaka kituo cha kurushia mchezo wao, hatimaye mazoezi hayo yameanza tena.
Kipemba alisema wanafanya mazoezi hayo kabla ya kuendelea kurekodi kazi hiyo tayari kwa kuanza kurushwa na moja ya vituo vya televisheni nchini ambacho hata hivyo hakupenda kukitaja jina kwa sasa kwa madai ni mapema mno.
"Muda ukifika wa kuanika jina la kituo hicho tutaweka bayana, ila tumeshaanza mazoezi ili kuendelea na kurekodi tamthilia yetu ya 'Kipusa' tuliyoizindua kwa mashabiki mapema mwaka huu," alisema Kipemba.
Kundi hilo linaloongozwa na Ndimbagwe Misayo Thea, linaundwa na wakali kama Muhogo Mchungu, Bi Hindu, Swebe Santana, Bi Staa, Bi Terry, Kingwendu, Davina na wengine.

Anti Fifii atengeneza Documentary ya maisha yake, kurusha hewani


NYOTA wa filamu nchini, Tumaini Biligimana maarufu kama Anti Fifii yupo hatua ya mwisho kutengeneza filamu inayohusu maisha yake (documentary) ya kisanii tangu alipoanzia sanaa hiyo mkoani kwa Kigoma hadi alipofikia sasa akiwa ni mtunzi, mwandishi, muongozaji na mtayarishaji.
Akizungumza MICHARAZO, Anti Fifii alisema kuwa kazi hiyo anayoitengeneza kupitia kampuni yake ya See Breeze Art ipo mwishoni kukamilika kabla ya kuanza mchakato wa kusaka mdhamini ili kurushwa hewani katika kituo chochote cha runinga watakachokubaliana nacho.
"Namalizia kutengeneza 'documentary' ya maisha yangu kuanzia nilipotokea kwetu Kigoma hadi kufika nilipo sasa na itarushwa kwenye runinga yoyote baada ya kukamilisha mchakato wa kupata wadhamini," alisema Fifii.
Nyota huyo wa filamu za 'Copy', 'Sound of Death', 'Senior Bachelor', 'I Deserve It', 'Kaburi la Mapenzi', 'Kizungumkuti', 'Fake Smile' na 'Daddy' alisema makala hiyo ya filamu itaenda kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Aidha aliongeza kuwa, anafanya mchakato wa kuweka kwenye makala ya filamu, kitabu chake kilichopo mtaani kinachoitwa 'Migogoro ya Ndoa na Suluhisho Lake'.
"Baada ya kukamilisha jambo hili, nitaanza mpango wa kutengenezea makala ya kitabu changu ili irushwe pia kwenye runinga kwa lengo la kuisaidia jamii," alisema.
Anti Fifii alisema anashukuru namna Watanzania walivyokipokea kitabu chake hicho cha kwanza kutunga nje na sanaa yake ya uigizaji aliyoianza miaka 20 Kigoma.

Yanga majanga tena, Fc Lupopo yaikoromea usajili wa Twite

WAKATI sakata la Emmanuel Okwi hata halijapoa, uongozi wa Yanga upo kwenye msukosuko mwingine baada ya viongozi wa klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kutua jijini na kudai kudhulumiwa fedha na klabu hiyo kupitia usajili wa Muyu Twite. Mmoja wa viongozi wa FC Lupopo, amesema Yanga walitakiwa kulipa dola 15,000 kama wamemuongezea mkataba Twite. "Lakini hawajafanya hivyo na nimekuja hapa viongozi wao Seif (Magari) na Abdallah (Bin Kleb) hawataki kulimaliza hili suala. "Mwanzo walisema hawataki maneno na sisi lakini mkataba unaonyesha mchezaji ni wetu na anacheza kwao kwa mkopo tu. "Kama waliona wanataka kuongeza mkataba lazima watulipe, tumewasiliana na chama chetu cha soka, ndiyo maana nimekuja hapa. "Lakini naona wanatuzungusha, tutasonga mbele hadi Fifa," alisema akisisitiza amefika hadi TFF lakini mambo yanaonekana ni magumu.
Bin Kleb alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kuwa atatoa ufafanuzi mara baada ya kutua Dar kwani alikuwa safarini.

Yazidu, Mualgeria kuzipiga leo Kilimanjaro

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjV3aoPNkQStbdya_xo9DDga_uJKAZONafyPywYx0IFQ9HWB7SawEnKhtxexF4oelIE9Lh6oDZ0boQqW0eMbWmi2A0pKrzwcbdX-ENAE9gZbMY8G-JDW69mvsv_K78nfdqdKonJ8QNLH2t9/s1600/IMG_1831.JPG
Said Yazidu (kushoto) ma Dahou wakiinuliwa mikono jana walipomaliza kupima uzito
BONDIA mkongwe nchini Said Yazidu wa Tanzania na Djamel Dahou kutoka Algeria wanatarajia kuonyeshana kazi leo kwenye pambano la kuwania Ubingwa wa Dunia wa UBO katika pigano litakalofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro.
Tayari Dahou ameshatua nchini tangu juzi tayari kwa pambano hilo la raundi 12 ambalo litafanyikia kwenye ukumbi wa YMCA, mjini Moshi na kusindikizwa na michezo mingine kadhaa ya utangulizi likiwemo la kuwania ubingwa wa UBO Afrika.
Mabondia wote wanaopanda ulingoni leo wamepimwa afya na uzito jana na wameonekana fiti tayari kurushiana makonde.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Anthony Rutta, pambano hilo la ubingwa wa Afrika litahusisha mabondia  Mtanzania Ali Ramadhan 'Alibaba' dhidi ya Mmalawi, Alick  Mwenda.
Ruta alisema mapambano yote hayo yameandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion na ni fursa nzuri ya kufufua ngumi za kulipwa katika mkoa wa Kiliamanjaro.
"Mpinzani wa Said Yazidu, Djamel Dahou ameshatua na anaelekea Kilimanjaro kwa ajili ya pambano lao la Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA," alisema.
Rutta alisema pambano hilo litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la UBO Afrika la raundi 10 kati ya Alibaba na Mwenda wa Malawi.
Mengine ni kati ya Fatuma Yazidu dhidi ya Joyce Adam, Emmanuel Alex dhidi ya Ali Bugingo huku Pascal Bruno atazipiga na Cosmas Kibuga, George Allen atazipiga na Ssebo Husseni na Raymond Bwango dhidi ya Fadhil Mkinda.

Kivumbi la michuano ya Pool Taifa kuanza kutimka leo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVwXLZSxMiJriebqbYIsPieAOIN6rLiBUHx9N4u0yJkAUGPLNzURJvSOxhHWQjOec3DeU8y34a52SMwhmYOjBE3PlSE7C_1CQfscSp88k5jk1XqRdpVuKuoy4Jrc5dLMysB74hTNkkpfaw/s640/DSC_0052.JPGFAINALI za Taifa za mashindano ya mchezo wa pool ya 'Safari Lager National Pool Championship 2014' zinazinduliwa leo mjini Kilimanjaro huku wachezaji wa timu zote 17 na viongozi wao wamewasili jana salama kwa ajili ya fainali hizo.
Katibu mkuu wa chama cha mchezo huo taifa (TAPA), Amosi Kafwinga aliliambia gazeti hili mkoani hapa kuwa taratibu zote zinazohusiana na fainali za mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager zimekamilika.
Kafwinga alisema wachezaji wa timu zote zitakazoshiriki fainali hizo tayari wamewasili huku kila timu ikitamba kutwaa ubingwa huo.
"Tunawashukuru wadhamini wetu bia ya Safari Lager kwa kufanikisha timu zote kuwasili kwa muda mwafaka huku kila kitu kinachohusiana na fainali hizo ikiwamo zawadi za washindi kikiwa kimekamilika," alisema Kafwinga.
Kafwinga alizitaja timu ambazo zitashiriki fainali hizo na mikoa yao ikiwa kwenye mabano kuwa ni Blue Leaf (Lindi), Yakwetu (Pwani), Billiard (Mwanza), New Stend (Shinyanga), Topland (Kinondoni), Absome (Tanga) na Corner Kasarani (Manyara).
Nyingine ni Mashujaa (Ilala), Tiptop (Tabora), Bilele (Kagera), Mboya (Kilimanjaro), Mpo Afrika (Temeke), Anatory (Morogoro), Delux (Dodoma), Ngija Point (Iringa) na Break Point (Mbeya).
Kafwinga alisema bingwa wa fainali kwa upande wa timu atajinyakulia fedha taslim Sh. milioni 5, kikombe na medali 10 za dhahabu, wakati kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) bingwa atazawadiwa Sh.500,000 na bingwa kwa upande wa wanawake ataondoka na Sh.350,000.
Naye nahodha wa mabingwa watetezi wa fainali hizo, Topland ya Kinondoni, Patrick Nyangusi akizungumza baada ya kuwasili mkoani hapa alisema lengo lao ni kutetea ubingwa wao na kurejea nao tena Dar es Salaam.
Nyangusi ambaye pia ni bingwa wa Afrika kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), alisema hakuna timu ya kuwazuia kuchukua tena ubingwa huo kutokana na maandalizi waliyoyafanya.
"Tumekuja  kutetea ubingwa wetu na tuna imani ya kurudi nao tena Kinondoni. Hakuna timu ya kutuzuia tumejiandaa vizuri, hivyo wadau wetu wa Kinondoni waondoe shaka tutawawakilisha vizuri na kurejea tena na ubingwa wetu," alisema Nyangusi.

Bayern Munich yapumua, Ribery arejea uwanjani

http://multimedia.pol.dk/archive/00430/Germany_Soccer_Bund_430303a.jpg
Franck Ribery
KLABU ya Beyern Munich imepumua baada ya wingawao Franck Ribery kuwa fiti baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa.
Winga huyo anatarajiwa kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wake wa msimu huu wakati timu yake itakapokwaana na VfB Stuttgart kesho Jumamosi.
Ribery amekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua lakini sasa anaonekana kuwa fiti. 
Mabingwa hao watetezi wameanza kwa kusuasua msimu huu kuliko ilivyokuwa kwa msimu uliopita kufuatia sare ya bao 1-1 dhidi ya Schalke katika mchezo wao wa pili. 
Kwa sasa wasiwasi upo kwa kiungo mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki Xabi Alonso ambaye alikosa mazoezi wiki hii kutokana na kuumia mguu na ndio kwanza maenaza kukimbia tena. 
Winga mahiri wa kimataifa wa Uholanzi, Arjen Robben naye pia amefanya mazoezi peke yake kutokana na majeruhi ya kifundo cha mguu wakati beki Rafinha naye akiwa bado nje kutokana na majeruhi ya goti.
Kurejea kwa Ribery ambaye mapema mwezi huu alitangaza kustaafu soka la kimataifa kunakuwa ahueni kubwa kwa Bayern kabla ya mechi yake ya kesho.

Ajabu! Wanne wakamatwa wakilima shamba uchi wa nyama

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/05/22a.jpg
Picha Haiuhusiani na habari hiyo
Na Faustine Fabian-Simiyu
JESHI  la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu wanne wa familia moja kwa tuhuma ya kukutwa wakilima uchi wa mnyama shambani kwa kile kinachodaiwa  kuwa ni imani za kishirikina.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Simiyu, Venansi Kimario alisema tukio hilo limetokea Sept. 2 majira ya saa 12 asubuhi katika kijiji cha Bushikwamala kata ya Kalemela wilayani Busega Mkoani Simiyu
Kimario alisema kuwa watu hao walikamatwa na jeshi la polisi alfajiri huko Bushigwamhala wakiwa wanalima kwenye shamba lao na walipohojiwa walidai kuwa walielekezwa na babu yao kipindi cha uhai wake kuwa wakilima uchi watapata mavuno  mengi.
Kamanda Kimario aliwataja waliokamatwa kuwa ni Makoye Kagoje (42), na mke wake Neema Kigwela (31) pamoja na watoto wao, mmoja wa kiume (15) na wa kike (12) majina yamehifadhiwa.
Aidha Kimario alisema watu hao pamoja na watoto wao wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa wakifanya vitendo vya ushirikina.
Babu yao alishafariki mwaka jana na aliwaambia kuwa wakilima wapo uchi watapata mavuno mengi, hivyo waliamua kufanya hivyo kutokana na wosia wa babu yao.
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema liliweza kufika katika eneo hilo na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kulima bila nguo.
Hata hivyo Kimario amewataka watu wasijishirikishe kwenye vitendo vya ushirikina na siyo kwamba ukilima uchi utapata mazao mengi tofauti na kufuata kanuni za kilimo bora, viongozi wa madhehebu ya dini na viongozi wa serikali tuwaelimishe watu waachane na imani za kishikina .

Thursday, September 11, 2014

BFT yasogeza mbele mashindano ya Taifa hadi Nov 3.

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/ngumilo.JPG?itok=lsVKoZrLMASHINDANO ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa yaliyokuwa yafanyike mwezi ujao yameota mbawa baada ya Shirikisho la mchezo huo nchini (BFT) kutangaza kuyasogeza mbele hadi Novemba.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga aliiambia MICHARAZO kuwa,  michuano hiyo iliyokuwa ianze kutimua vumbi lake kati ya Oktoba 8-14 sasa yataanza Novemba 3-8 kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
Mashaga alisema alisema wameamua kuahirisha michuano hiyo ili kupisha mashindano ya ngumi ya kimataifa yanayoandaliwa na Chama cha Ngumi cha wilaya ya Temeke (TABA) ambayo yatafanyika mwezi ujao.
Katibu huyo alisema wameona siyo busara kuendesha michuano ya taifa na mashindano hayo ya kimataifa ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Zantel.
"Tumeamua kuahirisha mashindano ya taifa ya ngumi hadi Novemba kupisha michuano ya kimataifa iliyoandaliwa na wanachama wetu mkoa wa Temeke, kuahirishwa huko kwa mwezi mzima ni fursa nzuri kwa mikoa kujipanga vema kabla ya kuja jijini Dar," alisema.
Mashaga alisema BFT inawatakia kila la heri timu za mikoa ambazo wameshawajulisha juu ya kuahirishwa kwa mashindano ya taifa, pia wakiipongeza Zantel kwa kujitolea kudhamini mashindano hayo ya kimataifa ya Temeke  kwa kutoa Sh. Milioni 10.
"BFT inawapongeza wadhamini wao na kuhimiza makampuni mengine kuiga mfano huo kwa lengo la kusaidia kuinua mchezo huo wa ngumi ambao umekuwa ukipambana kurejesha heshima ya Tanzania katika mazingira magumu," alisema Mashaga.
Katibu huyo wa BFT alisisitiza kuwa taratibu nyingine za mashindano ya Taifa yanaendelea kama kawaida na kwamba michuano hiyo itafanyikia kwenye uwanja wa Ndani wa Taifa.

Chicharito amvulia kofia Ronaldo, adai ni bora kuliko Messi

http://www.lapatilla.com/site/wp-content/uploads/2011/10/balon-de-oro-2011_323x216.jpg
MSHAMBULIAJI mpya wa Real Madrid, Javier Hernandez 'Chicharito' amesema tayari ameshawishika kwamba Cristiano Ronaldo ni bora zaidi ya Lionel Messi.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico amejiunga na mabingwa hao wa Ulaya kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Manchester United muda mfupi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Hata hivyo, Chicharito, ambaye alitua Old Trafford mwaka mmoja baada ya Ronaldo kutimkia Madrid, amesema tayari amedatishwa na mambo makubwa yanayofanywa na Mreno huyo mazoezini.
Bila ya shaka, Ronaldo ndiye bora," mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 aliliambia gazeti la El Chiringuito.
"Katika muda mfupi niliokuwapo hapa, nimemuona yeye ndiye bora zaidi duniani.
"Si kwamba hufanya vyema sana katika mechi tu bali hata kila siku.
"Kwangu mimi, Cristiano ndiye bora zaidi. Messi yuko matawi hayo pia; baada ya Cristiano, anafuatia Muargentina yule."

Mama Mkwe wa Jennifer Mgendi kutolewa Sept 22

FILAMU mpya ya muimbaji nyota wa Nyimbo za Injili nchini, Jennifer Mgendi iitwayo 'Mama Mkwe' itatolewa rasmi Septemba 22 mwaka huu.
Akizungumza na MICHARAZO, Mgendi alisema filamu hiyo iliyokamilika hivi karibuni akiwa ameigiza na wakali wa filamu na miondoko ya Injili akiwamo Mussa Banzi na Bahati Bukuku itatoka mtaani siku hiyo.
Mgendi amewataka mashabiki wa filamu wasiikose filamu hiyo kutokana na kubeba ujumbe mwanana wenye mafunzo makubwa kwa jamii.
Alisema filamu hiyo iliyoongozwa na Mgeni Khamis na Chrissant Mhega wa Mega  Video Production imekamilika wiki iliyopita.
Mgendi anayetamba na albamu ya Hongera Yesu, alisema ndani ya filamu hiyo inayozungumzia mkasa wa mama mkwe anayemlilia mwanae wa kiume kumletea mjukuu na kuzua kizaazawa wamo pia Senga,Bi Bi Esther, Christine Matai, Husna Chobis. yeye (Mgendi)  na wengine ambao wameinoigesha vilivyo.
"Nimekamilisha filamu yangu mpya ya 'Mama Mkwe' ambayo nimeigiza mimi, Bahati (Bukuku) Christine Matai, Senga, Bi Esther, Mussa Banzi na wengine. Ni filamu yenye mafunzo makubwa kwa jamii na hasa mama wakwe wanaoingilia ndoa za watoto wao," alisema.
Kabla ya filamu hiyo, Jennifer amewahi kutamba na filamu kadhaa kama 'Chai ya Moto', 'Joto la Roho', 'Teke la Mama', na 'Pigo la Faraja'.

Ruvu Shooting kupimana ubavu na 94 KJ Lugalo leo jioni

TIMU ya maafande wa Ruvu Shooting inayojiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo inatarajiwa kushuka dimba la Lugalo kuvaana na maafande wenzao wa 94 KJ katika mchezo wa kirafiki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na Afisa Habari wa timu hiyo, pambano hilo ni maalum kwa ajili ya kumpa nafasi kocha wao Mkenya Tom Olaba kuangalia mapunfugu wa kikosi chake dakika za mwisho mwisho kabla ya kujichimbia kuisubiri Ligi itakayoanza Septemba 20.
Timu hiyo ambayo ilimaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita ikilingana pointi na Simba na Kagera Sugar kila moja ikiwa na 38, inasema wanaamini timu hiyo ya 94 KJ iliyopo Ligi Daraja la Kwanza itawapa mazoezi ya kutosha vijana wao katika pambano hilo la leo.
Ruvu iliyoingia kambini tangu Juni 9 imekuwa ikichgeza mechi kadhaa za kirafiki tayari kwa ajili ya Ligi Kuu ambapo watafungua dimba kwa kuumana na maafande wa Magereza, Prisons Mbeya katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Mabatini.
Msimu uliopita walifungua dimba na wapinzani wao hao na kuwanyuka mabao 3-0, kitu ambacho Bwire anaamini hata msimu huu mambo yatakuwa hivi hivyo katika pambano hilo la ufunguzi wa ligi Jumamosi ijayo.

Wednesday, September 10, 2014

Hii ni ajali nyingine iliyotokea asubuhi ya leo Lindi na kuua wawili

2fru
Ni taarifa ambayo imethibitishwa pia na kamanda Mpinga na kweli imehusisha kifaru cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) saa kumi na moja alfajiri ambapo kifaru kimoja chenye tairi kwenye msafara wa jeshi hilo kimeripotiwa kuacha njia na kugonga nyumba.
Shuhuda alieongea na Power Breakfast ya CloudsFM amesema ‘Imetokea Mnolela kijijini Lindi kwenye msafara huu wa jeshi ilitangulia Iveco moja na nyuma vifaru viwili na walipofika kwenye eneo la shule kuna kona mbaya sana ambayo mara nyingi magari huwa yanaanguka’
‘Kifaru kimoja kwenye huo msafara kilikosa njia na kuingia bondeni kikagonga nyumba ya kwanza kikamkanyaga mwenye nyumba kikagonga nyumba ya pili kikazama kwenye hiyo sebule, kwa harakaharaka waliofariki ni watatu, Wanajeshi watatu na mwenye nyumba ya kwanza na wengine ni majeruhi wa hali mbaya kabisa’
1fru
‘Msafara ulikua unatokea Mtwara kuelekea Nachingwea kwenye kambi kuu, hii kona ni kali na aliejenga hii barabara amebakiza baadhi ya changarawe hakufagia kwahiyo mtu akikaribia changarawe zile mtu zinamvuta, hiki kifaru chenye tairi kilikua kwenye spidi kubwa sana usio wa kawaida ikamshinda ndio akatumbukia bondeni’ – Shuhuda
‘Mmoja wa waliofariki ni mama mwenye nyumba ya kwanza ambae alikua amelala kwenye chumba cha mbele ndio alikanyagwa na kufariki papohapo, walioumia ni Wanajeshi waliokua wamekaa juu ya kifaru hicho, wamepelekwa kwenye hospital ya Mkoa wa Mtwara’ – Shuhuda
Kamanda Mpinga amethibitisha kutokea kwa hili tukio, unaweza kubonyeza play hapa chini kumsikiliza shuhuda mwenyewe na kamanda Mpinga.
Kwa msaada wa Millardayo.com

Bondia Djamel Dahou atua kuzipiga Moshi na Yazidu

http://mfs0.cdnsw.com/fs/Root/8ak85-IMG_0187.JPG
Bondia Djamel Dahou atakayepigana na Said Yazidu siku ya Ijumaa
BONDIA Djamel Dahou kutoka Algeria ametua nchini alfajiri ya jana tayari kwa ajili ya pambano lake la kuwania ubingwa wa Dunia dhidi ya Said Yazidu wa Tanzania litakalofanyika kesho mjini Moshi, Kilimanjaro.
Pambano hilo la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa YMCA na kusindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la kuwania ubingwa wa UBO Afrika.
Pigano hilo jingin la ubingwa wa UBO litakuwa kati ya Mtanzania Ali Ramadhan 'Alibaba' dhidi ya Mmalawi, Alick  Mwenda.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST, litakalosimamia pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Green Hill Promotion, Anthony Rutta alisema Dahou alitua alfajiri ya jana kwa Ndege ya Egypt Airways.
"Mpinzani wa Said Yazidu, Djamel Dahou ameshatua na anaelekea Kilimanjaro kwa ajili ya pambano lao la Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA," alisema.
Rutta alisema pambano hilo litatanguliwa na michezo kadhaa ya utangulizi likiwamo la UBO Afrika la raundi 10 kati ya Alibaba na Mwenda wa Malawi.
Mengine ni kati ya Fatuma Yazidu dhidi ya Joyce Adam, Emmanuel Alex dhidi ya Ali Bugingo huku Pascal Bruno atazipiga na Cosmas Kibuga, George Allen atazipiga na Ssebo Husseni na Raymond Bwango dhidi ya Fadhil Mkinda.

Uholanzi yamtisha Sepp Blatter

http://vid.alarabiya.net/images/2014/07/27/837d0b74-5c15-435a-bd94-cc9250711bb9/837d0b74-5c15-435a-bd94-cc9250711bb9_16x9_600x338.jpgCHAMA cha Soka cha Uholanzi-KNVB kimedai kutompigia kura Sepp Blatter ambaye amethibitisha kugombea tena urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kipindi cha tano. 
Rais wa KNVB Michael van Praag aliwaambia waandishi wa habari kuhusu msimamo wao huo jana lakini akakiri kuwa haoni kama kuna mtu anayeweza kumng’oa Blatter katika nafasi hiyo. 
Uholanzi mara kadhaa wamekuwa wakimpinga Blatter mwenye umri wa miaka 78 ambaye alichukua madaraka hayo kutoka kwa Joao Havelange mwaka 1998. 
Katika mkutano mkuu wa FIFA uliofanyika nchini Brazil kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia, KNVB ilimpasha Blatter kuwa anatakiwa astaafu huku wakimtaka kuwajibika kutoka kashfa mbalimbali zilizolikumba shirikisho hilo. 
Lakini Blatter anaonekana bado kutaka kuendelea kukomalia nafasi hiyo kwa kipindi kingine kitakachomaliza mwaka 2019 akiwa na umri wa zaidi ya miaka 83, baada ya rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Michel Platini kuweka wazi kuwa hatagombea kiti hicho. 
Praag amesema bahati mbaya Platini amekataa kugombea kwani ndiye mtu pekee ambaye angeweza kusimama na Blatter.

Ramsey aiweka roho juu Arsenal

Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ball
Hobble: Ramsey is helped to his feet by a physio but he was unable to continue in Andorra
Twisted it: Chris Coleman says he hopes Ramsey's injury wasn't enough to keep him out for too long
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=6083#sthash.pLeuLv8H.dpuf
Going down: Ramsey picked up a suspected ankle injury while battling for the ballMASHABIKI wa klabu ya Arsenal wapo roho juu baada ya kiungo wao mahiri, Aaron Ramsey kuumia kifundo cha mguu na kuwa hatarisni kulikosa pambano la mwishoni mwa wiki dhidi ya Manchester City katika Ligi Kuu ya England.
Kiungo huyo alipata  majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa Wales wa mabao 2-1 dhidi ya Andorra jana usiku baada ya kufanyiwa rafu na mchezaji wa Andorra ambapo alipatiwa matibabu, lakini akatolewa uwanjani.
Meneja wa timu, Chris Coleman alisema ukubwa wa  majeruhi utatangazwa saa 24 kuanzia jana usiku, na hali hiyo imempa maumivu ya kichwa, kocha Arsene Wenger
Chris Coleman alisema anaamini majeruhi ya Ramsey haiwezi kumuweka nje ya uwanja wa muda mrefu.