TIMU za soka za Azam na JKT Oljoro zimezidi kupeta katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya jana kuendeleza wimbi la ushindi katika mechi zao zilizochezwa katika miji tofauti ya Dar na Arusha.
Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza
katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya
Azam katika mchezo huo yametiwa kimiani na Kipre Michael Balou wa Ivory Coast, dakika
ya tisa, Mganda, Brian Umony dakika ya 20 na Mkenya Humphrey Mieno dakika ya
46.
Bao la kufutia machozi la Toto lilitumbukizwa kimiani katika dakika ya 77 na Selemani Kibuta, ambalo hata hivyo halikuwaongezea lolote na kuifanya timu hiyo kupioteza mechi ya pili mfululizo kwa idadi ya mabao hayo 3-1.
Toto ililazwa idadi hiyo na Oljoro JKT katika mechi iliyochezwa mjini Arusha Jumamosi iliyopita, ambapo jana timu hiyo ya maafande wa JKT waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuilaza Kagera Sugar kwa mabao 2-0.
|
No comments:
Post a Comment