Emmanuel Okwi |
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi wa Simba anadaiwa kujiunga na klabu ya
Etoile du Sahel ya Ligi Kuu ya Tunisia kwa dola za Kimarekani 300,000 (Sh.
milioni 472).
Taarifa zilizopatikana jana jijini zinadai kwamba Okwi amekamilisha vipimo vya afya na kila kitu na tayari amesaini mkataba na klabu hiyo na atakuwa analipwa mshahara wa dola za Marekani 15,000 (Sh. milioni 24) kwa mwezi. Hata hivyo, haikuelezwa ni mkataba wa muda gani.

Taarifa hizo zinasema kuwa tayari Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameshatua nchini humo kwa ajili ya kuweka mambo sawa na kwamba sehemu za fungu hilo la usajili wa mchezaji huo zitagawanywa pia kwa klabu ya SC Villa kulingana na mkataba.
Okwi aliyekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba na ameachwa katika safari ya
Oman ambako mabingwa hao wa Tanzania Bara wameweka kambi kujiandaa na mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Baada ya
kumaliza mkataba wake wa awali na Simba Desemba mwaka jana, Okwi aliongeza
mkataba wa miaka miwili na ‘Wekundu wa Msimbazi’ ambao kabla hajaanza
kuutumikia, ameamua kuhamia Sahel.
Okwi akiitumikia timu ya taifa lake la Uganda |
No comments:
Post a Comment