MBUNIFU ALLY REMTULLAH KUIPEPERUSHA BENDERA MAREKANI
Meneja Masoko wa Kampuni ya
Tanzania Hair Industry ltd James Walwa – Jimmy akimkabidhi mbunifu wa
mavazi nchini Ally Rehmtullah tiketi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha
Afrika Mashariki katika mkutano wa ‘The Economics of the Africa Fashion
Industry’ utakaofanyika nchini Marekani mwezi wa Februari. Tanzania
Hair Industry ltd ambao ndio watengenezaji wa nywele maarufu aina ya
Darling ndio wadhamini wa safari ya mbunifu huyu kwenye mkutano huo wa
kihistoria utakaofanyika katika Kikuu cha Havard nchini Marekani.
Mbunifu
mahiri wa mavazi nchini Tanzania Ally Remtullah amechaguliwa
kuiwakilisha Africa Mashariki katika ‘East Africa Fashion Industry’
kuongea katika mkusanyiko wa Afrika Business Conference utakaofanyika
Harvard Business School nchini Marekani.
Akizungumza na Lenzi ya Michezo jijini
Dar es Salaam jana, Mbunifu huyo Remtullah amesema shughuli hiyo
itakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Marekani cha Harvard ambacho ni
kikubwa kuliko vyote duniani itafanyika Februari tarehe 15 mwaka 2013.
Akifafanua amesema kuwa kila
mwaka Chuoni hapo kunafanyika mikutano ya ‘Africa Business Conference’
ikiwa na kauli mbiu tofauti na sasa mwaka huu yeye amechaguliwa kuwa
mmoja wa wazungumzaji kuhusiana na ‘The Economic of Africa Fashion’.
Ally Remtullah amesema kwa
ujumla anaiwakilisha Afrika Mashariki katika kategori hiyo ambapo
anatarajiwa kuzungumzia changamoto zinazoikabili na fursa zinazopatikana
katika tasnia ya fasheni Afrika Mashariki, ikiwemo tatizo la umeme na
gharama za manunuzi ya vitambaa vya Pamba ambayo kimsingi huzalisha
katika ukanda huu.
Amesema anafurahi kuchaguliwa na
wandaaji hao kuziwakilisha nchi za Afrika Mashariki na sasa si kwenda
tena kuonyesha mavazi, bali ni kuzungumza mbele ya wadau wakubwa wa
kidunia kuhusu nafasi ya masuala ya ubunifu na uchumi.
Wazungumzaji wengine katika mkutano huo ni pamoja na mbunifu maarufu wa Afrika Magharibi Ituen Basi kutoka Nigeria.
Katika maandalizi hayo Ally
amesema pamoja na kusoma vitu vingi kuhusiana na uchumi katika tasnia ya
fasheni na gharama za uzalishaji za viwanda vya nguo, pia amekutana na
wafanyabiashara wakubwa wa viwanda vya kutengeneza nguo hasa za kiafrika
akiwemo Mfanyabiashara Mkubwa nchini Mh. Mohammed Dewji ambaye kwa
namna moja ama nyingine amempa ushirikiano wa kutosha.
Safari hiyo ya mbunifu wa mavazi
nchini Ally Remtullah katika mkutano mkubwa wa kihistoria wa Boston
nchini Marekani, imedhaminiwa na kampuni ya Tanzania Hair Industry Ltd,
ambao ni wazalishaji wa nywele maafuru aina ya Darling.
No comments:
Post a Comment